Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. dar
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema Chama cha Mapinduzi CCM na Serikali, hawatawafumbia macho watu wachache wanaokwamisha miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Ilala.
Mpogolo ameyasema hayo Februari 7, Mwaka huu katika ziara ya Kamati ya Siasa Wilaya ya Ilala, chini ya Mwenyekiti wake Said Side, iliyokuwa na lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo.
Wakitembelea miradi hiyo sita ikiwemo mradi wa kituo cha afya cha Mchikichini, barabara ya Pugu-Majohe,ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Gongo la Mboto iliyogharimu kiasi cha milioni 140, shule ya msingi Mizengo Pinda yenye madarasa matano, milioni 100,ituo cha afya cha Kinyerezi milioni 500 na shule ya sekondari Minazi Mirefu milioni 870.
Mpogolo amesema, fedha nyingi zimetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan, kwa ajili ya ukamilishaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, huku akidai kusua sua kwa miradi hiyo kunasababishwa na baadhi ya watu ikiwa pamoja na wakandarasi wasiyo na vigezo.
“Wapo watu waliokuwa wanakwamisha kukamilika kwake, hivi sasa chini ya Mganga Mkuu wa Wilaya na Mganga Mkuu wa kituo cha afya cha Kinyerezi tunawapongeza kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuhakikisha mradi huu sasa unakamilika,”.
Ameeleza kuwa tayari kituo hicho kina vitanda vinne kwa ajili ya wakina mama kujifungulia na vingine zaidi ya 10 vya kupumzika na gari ya kubebea wagonjwa, lakini pia vifaa tiba kwa ajili ya kutolea huduma tayari vipo.
‘Tuna kila sababu ya kuendana na kasi ya Rais na mnapoona CCM na viongozi wana hasira ni kwa sababu ya watu wa ngazi fulani wanatukwamisha hivyo ndani ya mwezi huu lazima jengo hili likamilike na huduma zianze,”amesema Mpogolo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Said Side, ameishukuru Serikali chini ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala na watendaji wake, kwa kuendelea kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni moja ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha CCM, huku akiomba miradi ambayo bado haijakamilika iendelee kusimamia ili iweze kukamilika kwa wakati.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi