Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Ilala
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo,ameishauri Halmashauri ya Jiji la Dar-es-Salaam, kutenga bajeti ya kutosha eneo la mazingira pamoja na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Mpogolo amesema hayo Februari 12,2025,wilayani Ilala katika kikao cha ushauri Wilaya (DCC), kilichofanyika jijini Dar- es-Salaam.amesema ametoa ushauri huo kwa sababu Ilala imekuwa ikiongoza kupokea wageni wengi, hivyo mazingira yanatakiwa kuendelea kuboreshwa, kutoka uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere hadi katikati ya Jiji.
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250212-WA0014-1-703x1024.jpg)
“Rais amekuwa ‘champion’ wa matumizi ya nishati safi ya kupikia,umefanyika mkutano unaohusu masuala ya nishati, yote haya yanaonesha namna Serikali ilivyojipanga katika eneo hili,ndiyo maana tumeshauri Halmashauri ya Jiji letu kwenda na kauli mbiu ya Serikali kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi,”amesema Mpogolo.
Pia Mpogolo amesema,maandalizi ya soko la Kariakoo kufanya biashara kwa saa 24 mchakato wake unaendelea vizuri na wafanyabiashara wamepokea vizuri uamuzi huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Elihuruma Maberya,amesema Ilala inatarajia kukusanya kiasi cha bilioni 140, katika mwaka wa fedha wa 2025 /2026 ikiwa ni ongezeko la asilimia 10 kulinganisha na bajeti ya sasa.
Maberya amesema asilimia 70 ya bajeti hiyo itakwenda kuhudumia wananchi katika miundombinu ya afya,elimu na barabara pamoja na kuwawezesha kiuchumi.
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250212-WA0013-1.jpg)
More Stories
Dkt.Mpango aagiza mfumo wa NeST utumike kudhibiti ubadhirifu,aipongeza PPRA
DC Malisa ataka taarifa mahudhurio ya wanafunzi
Sheria mpya nguzo ya uwekezaji kuongezeka nchini