Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
MGOMBEA kiti cha Rais kutoka Chama cha ACT Wazalendo,Luhaga Mpina amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo katika Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) huku akidai wataanza kutafuta wadhamini katika Kijiji cha Mwandoya katika Jimbo la Kisesa mkoani Simiyu ambapo ndipo alikozaliwa.
Mpina Akiwa na mgombea mwenza Fatma Abdulhabib Ferej alizungunza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi hiyo ambapo amesema kinachofuata mara baada ya uchukuaji fomu ni kutafuta wadhamini ambapo amewaomba wananchi kujitokeza kukidhamini Chama hicho.
Amesema baada ya Simiyu wataanza kutafuta wadhamini katika maeneo mengine huku akidai mara baada ya kupata wadhamini ndipo atazungumzia vipaumbele vya Chama hicho.
“Niwaombe vijana wajitokeze kwa wingi ili tupate sifa na hawatafuata mambo ya Vyama,”amesema Mgombea huyo.






More Stories
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi