Na Hadija Bagasha, Timesmajira Online,Tanga
CHAMA cha Ushauri wa Wanafunzi wa vyuo vikuu na vya kati Tanzania (TACOGA 1984),kinafikiria kushirikisha taasisi za elimu ya chini, kwenye mpango wa kujenga kizazi chenye maadili.Kuanzia elimu ya awali,msingi hadi vyuo vikuu, hatua hiyo inayokuja mara baada ya kubainika maadili kwa jamii yameporomoka.
Hayo yameelezwa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Mdhibiti Mkuu Ubora wa shule Kanda ya Kaskazini Mashariki,,Akwila Sawaya, mkutano wa TACOGA 1984,unaofanyika jijini Tanga,ili kujadili masuala mbalimbali ikiwemo ya jinsia na elimu jumuishi kwa wanafunzi.
Amesema, vyuo vikuu vinaweza kushiriki kujenga kizazi chenye maadili na kinachoweza kuwa msaada kwa taifa.Pia wanaamini watafanya kazi ya kurejesha vijana kwenye tamaduni zinazokubalika,hivyo kusaidia kupata viongozi na wataalamu wazuri wenye maadili na wanaofata tamaduni za Tanzania.
“Lengo kubwa ni kuhakikisha elimu jumuishi inakuwepo,pia suala la maadili na tamaduni zetu zinazingatiwa kwa vijana wetu.Kinachotakiwa ni kushirikisha taasisi za elimu ya chini,kwani tunahitaji elimu wanayotoa ifike kwa vijana na watoto kuanzia shule za awali, msingi na sekondari,”.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA),Prof. Mohamed Makame Haji, ambaye ni mjumbe wa bodi ya wadhamini wa chama hicho, amesema mkutano huo unaangalia kwa namna gani chama hicho, kinaweza kuwa sehemu kuu ya kutengeneza wanafunzi na kuwa raia wema wanapohitimu mafunzo yao.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM),Prof.Lughano Kusiluka ,amrsema jamii inatakiwa kusadia kujenga kizazi chenye maadili,baaada ya dalili zilizopo kuonesha maadli yameporomoka kwa vijana.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakani
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best