December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Viongozi wa CHADEMA wakiwa kwenye kikao cha Kamati Kuu

Moshi mweupe kumpata mgombea urais CHADEMA waanza kufukuta

Na Mwandishi Wetu

KIKAO cha Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinaendelea vizuri kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Kuanza kwa kikao hicho ni hatua ya kwanza ya mchakato wa kumtafuta mgombea urais atakayepeperusha bendera ya chama hicho kwenye kinyang’anyiro cha urais katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba, mwaka huu.

Viongozi wa juu CHADEMA wakifuatilia hoja za wajumbe wa kikao hicho
Kikao kikiendelea

Kesho Agosti 3, kitafanyika kikao cha Baraza Kuu mkutano ambao utahudhuriwa na wajumbe 600 na keshokutwa Agosti 4, ni Mkutano Mkuu ambao wajumbe wake ni 1,500.