Na Moses Ng’wat, Timesmajira Online,Momba.
HALMASHAURI ya Wilaya ya Momba imetajwa kuibuka kinara wa ukusanyaji mapato ya ndani kwa robo ya kwanza ya mwaka wa 2023/2024, baada ya kufanikiwa kukusanya kwa asilimia 54 ya malengo waliyojiwekea.
Hayo yalibainishwa na Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Happiness Seneda, Septemba 10,2023, wakati akizungumza na Watumishi wa Halmashauri hiyo na kuwapongeza kwa kufanya kazi kwa mshikamano.
Ambapo hali hiyo imewezesha kufikisha asilimia 54 na kuwa kinara ukilinganisha na halmashauri nyingine za Mkoa wa Songwe.
“Nikupongeze Mkurugenzi Mtendaji na timu yako licha ya changamoto ya uhaba wa watumishi lakini mmejipanga vizuri na mmefanikiwa kukusanya mapato ya ndani kwa ufanisi mkubwa jambo ambalo kipindi cha nyuma haikuwa hivyo, endeleeni na ushirikiano na mshikamano huo ili msonge mbele zaidi,”amesema Seneda.Â
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Regina Bieda amesema licha ya kupongezwa watahakikisha wana ongeza jitihada ili wakusanye zaidi ambapo katika mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri hiyo iliweka makisio ya kukusanya kiasi cha bilioni 1.8.
Amesema hadi kufikia Oktoba 30, 2023, Halmashauri imekusanya kwa asilimia 54, hali ambayo amedai imewapa matumaini makubwa ya kuvuka lengo.Â
Ikumbukwe kuwa, RAS Seneda yupo kwenye ziara ya kukagua miradi ya maendeleo kwenye Tarafa zote mkoani humo ambapo ameanza na Halmashauri ya Tunduma, Mbozi na sasa yupo Momba.
More Stories
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi
Mwanasiasa mkongwe afariki Dunia
Rais Samia Kuzindua Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo