November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

MoCU waiunga mkono serikali kwa kutoa Elimu bora

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), kimeendelea kumuunga mkono Waziri wa Elimu Prof. Adolf Mkenda na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutoa elimu bora kwa wanafunzi wake.

Akizungumza wakati wa maonesho ya Vyuo Vikuu yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es salaam, Dkt. Faustine Panga kutoka Chuo Kikuu cha Ushirika (MoCU), amesema kwa kuwa chuo chao ni cha serikali ada yao imekua ni nafuu na mazingira ni bora zaidi kwa mwanafunzi kupata elimu;

“Mazingira ni mazuri, ada ni nafuu ambapo kwa degree ni Milioni moja na laki moja kwa mwaka mmoja, cheti ni laki saba na Masters ni milioni mbili na nusu kwa mwaka hivyo karibuni wote mje mpate elimu iliyo bora” Amesema Panga.

Aidha panga amezitaja programu zinazopatikana katika chuo hicho kikuu cha Ushirika Moshi;

“Chuo chetu kinatoa programu ngazi ya Cheti, Diploma, Degree na PDH , na katika maonesho haya udahili ni bure “

Pia Panga alisema mbali na Moshi wana ofisi za mikoa 13 ambayo inatoa shughuli za kuhudumia vyama vya ushirika, wapo mkoani Shinyanga, kizumbi na wanatoa programu ya cheti na diploma na kwa moshi ni Certificate, Diploma na Degree zote.

Panga alisema Chuo hicho wana kliniki ya maendeleo ya ushirika hivyo kama kuna wadau wa ushirika ambao wapo Dar es salaam kwa sasa na vyuo vyenye vyama vya ushirika wafike katika maonesho hayo ambapo yupo mtaalamu wa ushirika ambaye anatoa huduma ya namna ya kuboresha lakini pia wanatoa rufaa ya nani atakayeweza kushughulikia suala la mteja ambapo ikitokea wameshindwa kutatua huduma ya mteja aliyokuwa akiihitaji wanamuelekeza wapi pa kwenda kupata huduma hiyo.

Kuhusu Mapokeo katika maonesho hayo Panga amesema ni mazuri, watu wengi wameshafika kujisajili na kupata maelezo na wengine wanaendelea kufika kupata huduma mbalimbali wanazozitoa.