Na David John
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imemkamata kigogo wa dawa za kulevya raia wa Nigeria, Kanayo Chukwu (39) mkazi wa Masaki jijini Dar es Salaam akiwa na dawa za kulevya aina ya heroin zinazokadiriwa kuwa na zaidi ya kilogramu 270.
Mbali na Chukwu, mamlaka hiyo pia inawashikilia raia wawili wa Tanzania, Alistair Mbele (38) ambaye ni Mkutubi wa Chuo Kikuu cha Aghakan jijini Dar es Salaam, mkazi wa Mbezi Kibanda cha Mkaa na Isso Romward Lupembe (49) mkazi wa Mbezi Louis na Changanyikeni jijini ambao wanadaiwa kufanya biashara hiyo kwa kushirikiana na raia huyo wa Nigeria.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo, James Kaji, alisema watuhumiwa hao walikamatwa April 15,2020 na wamekuwa wakifanya biashara hiyo kwa muda mrefu nchini.
Alisema mamlaka imefanikiwa kuwakamata watu hao kutokana na jitihada na ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na nchi nyingine katika kupambana na tatizo la dawa za kulevya duniani, hasa utaratibu wa kubadilishana taarifa ambazo husaidia kurahisha ukamataji huo.
Kaji alisema “Watuhumiwa walikamatwa na dawa za kulevya aina ya heroin zinazokadiriwa kuwa na zaidi ya kilogramu 270 zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye moja ya nyumba iliyopo Mbezi kibanda cha mkaa,” alisema Kaji
“Baada ya kupata taarifa kutoka kwa vyombo mbalimbali vya usalama ndani na nje ya nchi tulianza kuwafuatilia tangu Aprili 8, mwaka huu na kufanikiwa kuweka mtegoni tangu wakiwa wanashusha mzigo na ndipo tulipofanikiwa kuwakamata.”alisema Kamishna Kaji
Taarifa kamaili kwenye gazeti la Majira…
More Stories
Mhandisi Samamba awasisitiza maafisa madini kusimamia usalama wa migoni msimu wa mvua
Wapinzani kutimkia CCM ishara ya ushindi Uchaguzi Serikali za Mitaa
Vikundi Ileje vyakabidhiwa mikopo ya asilimia 10, DC Mgomi avipa somo