November 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Zuhura Mawona-Kaimu Mkurugenzi wa Uuguzi Muhimbili

MNH kuendelea kutambua mchango wa wauguzi

Na Penina Malundo

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili imeendelea kutambua mchango mkubwa unaofanywa na wauguzi katika sekta ya afya kwa kuendelea kufadhili masomo kwa wauguzi mbalimbali wanaojiendeleza ndani na nje ya nchi ili kuboresha huduma za kibingwa zinazotolewa katika hospitali hiyo kubwa nchini.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Uuguzi, Zuhura Mawona katika mkutano wake na waandishi wa habari katika kuadhimisha siku ya wauguzi duniani iliyobeba kauli mbiu isemayo; Wauguzi; Sauti inayoongoza Uuguzi kwa Dunia yenye Afya.

Mawona amesema ili kuhakikisha usalama wa watoa huduma hasa katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa homa ya mapafu COVID19, Kurugenzi ya Uuguzi na Ukunga katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kupitia kitengo cha ushonaji hivi karibuni imebuni na kushona mavazi ya watoa huduma  kujikinga na maambuzi (PPE)

“Kurugenzi ya Uuguzi na Ukunga katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, kupitia kitengo chake cha ushonaji, imeendelea kutengeneza vifaa kinga (MNH PPE GOWN) kwa ajili ya kuwakinga watoa huduma wanao hudumia wagonjwa walioambukizwa COVID 19, ambapo awali mavazi hayo upatikanaji wake ulikuwa adimu.” Amesema
 Mawona

Kwa habari zaidi soma Majira kesho