Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online,Kisesa Meatu
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (MNEC) Mkoa wa Simiyu, Emmanuel Gungu ametoa pikipiki mbili kwa askari wa Wanyamapori wa Pori la Akiba Maswa Jimbo la Kisesa ili kusaidia kuongeza nguvu ya kuwadhibiti wanyama wakali huku akiwataka viongozi wa kuchaguliwa na wananchi kutatua kero za wananchi wao sio kuwa watu wa kulalamikia serikali.
Kwani viongozi hao wanajua jinsi serikali inavyoleta maendeleo kwa wananchi ambapo ametoa pikipiki hizo mara baada ya kupokea, maombi ya kuwasaidia wananchi wa Jimbo hilo ambao bado wanasumbuliwa na Tembo na kuharibiwa mali, chakula na makazi yao.
Hata hivyo, kabla ya kukabidhi pikipiki hizo, akizungumza katika mkutano huo na viongozi hao wa Jimbo la Kisesa, Gungu amewataka viongozi wa kuchaguliwa na wananchi, waache kuilalamikia Serikali na kuisema kila kukicha, kwani wao kazi yao nikuhakikisha wanawasikiliza wananchi na kusikiliza kero zao pamoja na kuzitafutia ufumbuzi.
“Katibu wa Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina amewasilisha maombi kwamba watu wanacheleweshwa kulipwa fidia, kwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa, “Naomba nikwambie ukwamwambie Mbunge suala hilo lipo mikononi mwake, kwani Mbunge ndio anaetunga sheria, kusimamia sheria na kuwaelimisha wananchi, hivyo yeye atusaidie kwakuwa wao ndio wanaotunga sheria hizo,”amesema Gungu na kuongeza kuwa
“Hata Diwani wetu wahapa Tindabuligi unanafasi ya kutusaidia huko kwenye Serikali, kumaliza changamoto za Wananchi sio mnalalamika tu jamani mtusaidie, muwasaidie wananchi,unaingia kwenye vikao vya Halmashauri unauwezo wa kupigania mambo ya maendeleo ya wananchi na yakafanyika,”amesema Gungu.
Gungu amesisitiza kwamba lazima viongozi wamsaidie Rais kutatua changamoto za Wananchi ambazo zipo ndani ya uwezo wao na kwamba sio kila kitu lazima afanye yeye wakati wasaidizi wake wapo.
Kupitia mkutano uliyowakutanisha Makatibu Kata, Madiwani na Wananchi wa Jimbo la Kisesa Mnec huyo pia ameahidi kuzungumza na wadau wengine ili kusaidia kupatikana kwa pikipiki nyingine zisizopungua 10.
Ofisa Mhifadhi wa Pori la Akiba Maswa, Lawrence Okode amemshukuru Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa kwa kusaidi kununua Pikipiki mbili ambazo ameeleza kuwa zitakuwa msaada mkubwa wa kupunguza usumbufu kwa Wananchi kushambuliwa na Tembo.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Tindabuligi, Tabu Maghembe amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha bilioni 1.8 kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Kata ya Tindabuligi.
More Stories
Hatma mrithi wa Kinana kupatikana
Mrithi wa Kinana CCM kujulikana katika Mkutano Mkuu wa Jan 18/19
Wananchi Kiteto waishukuru Serikali,ujenzi wa miundombinu ya barabara