Na Esther Macha , Timesmajira Online ,Mbeya
MJUMBE Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Chama Cha Mapinduzi(CCM),Mkoa wa Mbeya , Ndele Mwaselela amesema chama hicho kimetengeneza uzio kuhakikisha Dkt.Tulia Ackson anapata kura za kishindo katika uchaguzi Mkuu 2025.
Amesema hawatoruhusi watu kuchukua fomu ya kuwania nafasi wala kupenyeza kuingia kwenye kinyang’nyiro ifikapo 2025 kwani tayari wameweka uzio katika nyanja mbalimbali.
Mwaselela amesema hayo Aprili 8, mwaka huu wakati akitoa salamu kwenye Iftar iliyoandaliwa na Taasisi ya Tulia Trust chini ya Mkurugenzi wake mbaye ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini na Spika wa Bunge Dkt.Tulia Ackson jijini hapa .
Aidha Mwaselela amewataka wananchi na waumini mbalimbali waliohudhuria Iftar hiyo kuwaelimisha watu wenye vichwa vigumu mazuri yaliyofanywa na Dkt.Tulia na yanayoendelea kufanywa ili wote waweze kwenda pamoja 2025.
Hata hivyo Mnec huyo amewaomba viongozi wa dini mkoani Mbeya kuendelea kumuombea Dkt.Tulia kutokana na kuubeba Mkoa ili mambo mengine yaendelee kuwa mazuri zaidi.
Mgeni rasmi katika Iftar hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Juma Homera amesema kuwa utendaji kazi na kujitoa kusaidia wenye uhitaji kwa Dkt. Tulia ni darasa na chuo tosha kwa viongozi wengine katika kuhakikisha wanajikita kuwahudumia wanadamu kwa moyo wa upendo .
“Amegusa sekta zote ikiwemo elimu,afya,maji ,nishati, miundombinu uimarishaji wananchi kiuchumi na uhusiano katika jamii tunapozungumzia kama mnavyoona hapa tumekutana dini zote tunapata Iftar,”amesema Homera.
Sambamba na hilo pia Dkt.Tulia ametoa vifaa vya shule kwa kata 36 kwa wanafunzi wenye uhitaji ndani ya Mkoa wa Mbeya kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari,sare kwa wanafunzi wenye uhitaji zaidi ya 3000 kwa shule za msingi .
Shekhe wa Mkoa wa Mbeya, Msafiri Njalambaha amesema kuwa wamekuwa wakiona viongozi wengine wakiandaa futari lakini mwasisi ni Dkt.Tulia kwani amekuwa anafanya kwa ajili na sio masuala ya kisiasa.
Amesema yapo mambo mbalimbali ambayo ameyafanya ikiwepo ujenzi wa misikiti katika Wilaya ya Rungwe, Kiwira ,Msikiti na Uyole sambamba na kutoa vifaa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la ofisi ya Bakwata.
“Mambo tofauti yanapotokea anakuwa wa kwanza kufika tulishuhudia watu walipopata matatizo aliwajengea nyumba nilisema haya anayofanya Dkt.Tulia sio kwamba anafanya sababu ni mwanasiasa bali anafanya sababu Mwenyezi Mungu amemumwekea kitu ndani ya moyo wake ,nasema huyu ni kiongozi ambaye lazima twende nae sambasamba,”amesema Shekhe Njalambaha.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi