Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa(MNEC)Ndele Mwaselela amewataka wanasiasa kutumia ndimi zao vyema katika majukwaa yao na kuepuka kutumia ndimi hizo kuwa moto kwa Taifa na kuiharibu amani ya Nchi.
Mwaselela amesema hayo Juni,22,2025 wakati aliposhiriki Ibada ya kuliombea Taifa la Tanzania na Viongozi wote wakiongozwa na Rais Dkt.Saimia Suluhu Hassan ibada iliyofanyika katika ukumbi wa mkapa Jijini Mbeya.
“Tunapoelekea Kwenye uchaguzi mkuu Ndugu zangu wanasiasa tuepuke kutumia ndimi zetu vibaya katika majukwaa yetu kwa maana yanaweza kuharibu amani ya nchi yetu “amesema Ndele Mwaselela.
Akiendelea kuongea katika maombezi ya kuliombea Taifa MNEC Mwaselela amewaomba watumishi na waumini wote kuombea amani nchi pamoja na Rais ili mwenyezi Mungu amwongoze kwa kadri mapenzi yake na hekima katika Taifa letu.
Aidha Mwaselela amesema kuwa wanaenda kwenye Uchaguzi kama CCM kinaenda kushindana hivyo ni lazima kumuomba Mungu ili kuweza kupata viongozi wenye hofu ya Mungu kama ilivyo kwa Rais wetu.
“Tuna kila sababu za kuhakikisha tunafanya maombi ili kuweza kupata viongozi walio bora na siyo bora viongozi,tuchague viongozi wenye maono ambao watakisaidia chama cha Mapinduzi katika kutatua changamoto za wananchi “amesema MNEC Mwaselela.
Hata hivyo Mwaselela amechangia Kiasi cha shilingi Mil.2 kwa ajili ya huduma ya Uimbaji na Uinjilishaji Katika Mkoa Wa Mbeya.


More Stories
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi