Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online,Simiyu
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa, (MNEC) Mkoa wa Simiyu, Emmanuel Gungu ametoa vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya milioni 10 kwa watu wenye mahitaji maalum kwa Wilaya zote za Mkoa wa Simiyu.
Pamoja na kwenye Magereza yote yaliyopo katika Wilaya tano za Mkoa huo, ili kusherekea vema Sikukuu ya Idd.
Gungu ametoa vitu hivyo wakati akishuhudia mashindano ya kusoma Quran katika Msikiti Mkuu wa Bakwata wilayani Bariadi mkoani Simiyu, ambapo amesema lengo ni kuwezesha waumini wa dini ya Kiisilam wa Mkoa huo na watu wenye uhitaji kusherekea vema sikukuu hiyo.
“Nimetoa mchele kwa Wilaya zote za Mkoa wa Simiyu,maharage,mafuta,tende na nguo aina ya kanga kwa wafungwa wanawake, nimewakumbuka na ndugu zetu waliopo kwenye Magereza yote ya Mkoa wetu wa Simiyu, watapata vitu kama nilivyovitoa kwa wengine,”amesema Gungu.
Gungu ameahidi kushirikina na Waislamu katika kudumisha amani, umoja na mshikamano na kumuunga mkono Rais Samia ili kuhakikisha Mkoa wa Simiyu unakuwa katika nyanja mbalimbali za maendeleo na kiuchumi.
Kwa upande wake Shekhe wa Mkoa wa Simiyu, Shekhe Issa Kwezi alimshukuru Mjumbe huyo wa Nec kwa msaada wake huo, ambapo amesema utawawezesha watu wenye uhitaji kusherekea vema sikukuu ya Idd pamoja na Waislamu wote wa Mkoa huo.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Faiza Salim akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Daktari Yahaya Ismail Nawanda amewapongeza vijana waliyoshiriki katika mashindano hayo ya kusoma Quruan na kuwataka Wazazi na Walezi kuwalea watoto wao katika maadili yaliyo mema.
More Stories
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Baraza la Taifa la Ujenzi waingia makubaliano ya mashirikiano sekta ya ujenzi
Nderiananga aongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa tatu wa Kimataifa wa watu wenye ulemavu ujerumani
Taarifa za maendeleo ziwafikie wananchi kwa usahihi