Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Taifa, Khamis Hamza Chilo,amewataka wana CCM wilaya ya Ilala kuondoa makando kando na kujenga mshikamano kuakikisha CCM inashika dola.
MNEC Khamis Hamza Chilo alisema hayo kata ya Ilala katika mkutano mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya chama cha Mapinduzi ulioandaliwa na kamati ya Utekelezaji kata ya Ilala.
“Nawaomba wan CCM wezangu muondoe makundi na Mkanganyiko ndani ya chama chetu kiweze kushinda na kushika dola hivyo tuache makundi na makando kando “alisema MNEC Khamis .
MNEC Khamis Hamza Chilo alisema chama cha Mapinduzi uhai wake ni wanachama, CCM ina wenyewe na wenyewe ndio sisi kwa ushirikiano wa umoja wetu katika kujenga chama na jumuiya zake.
Aliagiza umoja na mshikamano uendelezwe ili CCM iweze kusonga mbele na kushinda kwa kujenga umoja na mshikamano itashinda katika chaguzi za Serikali za mitaa.
Alisema uongozi anapanga Mwenyezi Mungu hivyo amewataka wana Ilala kumpa ushirikiano Mbunge wa jimbo la Ilala ambaye ni Naibu Spika Mussa Zungu na Diwani wa Ilala Saady Khimji kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM vizuri ambapo kata ya Ilala utekelezaji umefanyika vizuri wa miradi ya maendeleo vikiwemo vituo vya afya,Barabara, na sekta ya Elimu
MNEC Khamis Hamza Chilo akizungumzia Jumuiya ya Wazazi ya CCM kata ya Ilala ina jukumu kubwa la kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM katika kusimamia miradi ya maendeleo.
Alipongeza Jumuiya ya Wazazi kata ya Ilala kwa kuandaa mkutano mkuu pamoja na kufanya kazi kubwa ikiwemo kusaidia jamii ya eneo la kata ya Ilala
Aliagiza Jumuiya ya Wazazi kata ya Ilala kulinda watoto na kusimamia maadili ikiwemo kufatilia matokeo yao kitaaluma shuleni kwa kushirikiana na walimu .
Aliwataka Wazazi kwenda kusimamia sekta ya Elimu ili waweze kupata viongozi bora wa Taifa la kesho ambalo litaibua mawaziri na Rais waje kusaidia chama cha Mapinduzi.
Wakati huohuo MNEC Khamis Hamza Chilo aliwataka Jumuiya ya wazazi wajiandaae kwa ziara maalum ya kwenda Zanzibar ambayo anatarajia kuwapa mwaliko rasmi hivi karibuni kwenda kujifunza.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kata ya Ilala Sabry Sharif alisema Jumuiya ya Wazazi Kata ya Ilala inafanya kazi zake za Jumuiya vizuri kwa kushirikiana na kata na ngazi ya Kata na Wilaya.
Mwenyekiti Sabry alisema chama cha Mapinduzi CCM chama bora kina jenga uhusiano bora wanafanya kazi kwa ushirikiano katika kujenga chama na Serikali.
Katika hatua nyingine Jumuiya ya Wazazi Kata ya Ilala ilitoa zawadi maalum ya Mgeni rasmi Mjumbe wa Halmashauri Kuu MNEC Taifa Khamis Hamza Chilo pamoja na zawadi maalum kwa Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mbunge wa jimbo la Ilala Mussa Zungu.
More Stories
HGWT yawarejesha kwao wasichana 88 waliokimbia ukeketaji
Sherehe Miaka 61 ya Mapinduzi Zanzibar zafana
Simbachawene:Waombaji wa ajira jiungeni na Mfumo wa Ajira Portal