Na Mwandishi wetu,Timesmajira
MNADHIMU Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Othman Othman, amewapongeza Maafisa na Askari wa kikosi cha Polisi Jeshi waliomaliza jukumu lao la ulinzi wa amani nchini Lebanon.
Akitoa pongezi hizo leo jijini Dar es Salaam wakati akipokea Bendera ya Taifa kutoka kwa Askari wa kikosi hicho, katika hafla iliyofanyika katika Chuo cha Ulinzi wa Amani Tanzania kilichopo Kunduchi.
Luteni Jenerali Othman amesema kuwa kikosi hicho kimeiwakilisha vyema Tanzania katika jukumu la kimataifa la kulinda amani, na kwamba nidhamu, uzalendo na ufanisi wao katika kazi vimetoa heshima kubwa kwa taifa.
“Ninyi mmekuwa mabalozi wazuri wa Tanzania,mmeonyesha mfano bora wa ushiriki wa nchi yetu katika kulinda amani duniani.

“Nachukua nafasi hii kuwapongeza kwa moyo wa ujasiri na kujitolea mliouonyesha mkiwa nje ya nchi kwa muda mrefu,”amesema Luteni Jenerali Othman.
Aidha, amesisitizakuwa umuhimu wa kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa katika masuala ya amani na usalama, huku akiwasihi askari hao kutumia uzoefu walioupata nchini Lebanon katika kuboresha utendaji kazi wao hapa nyumbani.

Kikosi hicho kilikuwa sehemu ya Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Ulinzi wa Amani nchini Lebanon (UNIFIL), ambapo kilishiriki kwa mafanikio katika kuhakikisha usalama na utulivu katika maeneo ya mgogoro

More Stories
Wanawake washauriwa kuchangamkia fursa za uchumi
Aida:Wanawake wakipata haki zote itapunguza migogoro
LGTI wanawake waadhimisha siku yao Ngorongoro