Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya
JAMII na wadau mbalimbali Jijini Mbeya wameombwa kumuunga mkono Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini ,Rais wa IPU Dkt.Tulia Askson katika jitihada zake za kusaidia watu wasiojiweza na wenye uhitaji ikiwemo Makazi ,malazi na chakula .
Kauli hiyo imetolewa leo na Hosea Kalumelu mkazi wa mtaa wa Nyibuko kata ya Mwakibete mkoani Mbeya ambaye ni Mlemavu wa Macho asiyeona wakati wa kukabidhiwa nyumba yenye vyumba viwili na sebuleni na Rais wa umoja wa Mabunge duniani na Spika wa Bunge (Mb)ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa hivi karibuni baada ya kuombwa na mhitaji Hosea.
Kalumale amesema kuwa kwa kazi kubwa inayofanywa na Dkt.Tulia ipo haja ya kuunga mkono na watu wengine na kuwa kazi anayofanya kusaidia wahitaji asifanye peke yake kwani anafanya jambo kubwa la baraka .
“Unajua katika mkoa wa Mbeya na wilaya zake wangekuwa na moyo kama wa Dkt.Tulia kila pande zote za mkoa huu wangeng’ara sasa shida wenye mioyo kama hii kuwakuta ni kazi kubwa na unapotoa hazina yako inaongozeka Sasa hivi nimekabidhiwa nyumba hii ya kuishi yenye vyumba viwili na sebule na choo cha kisasa nashukuru Sana Dkt.Tulia “amesema Kalumelu.
Kwa upande wake Rais wa umoja w mabunge duniani ambaye ni Spika wa Bunge na mbunge wa jimbo la mbeya mjini Dkt.Tulia Ackson amesema kuwa matamanio yake ni kuona watu wenye uhitaji wanasaidiwa na kwamba hiyo ni nyumba ya tisa kukabidhiwa na Taasisi ya Tulia Trust.
Dkt.Tulia amesema kuwa wahitaji wapo wengi na angetamani kuwafikia wengi hivyo na kuwataka wananchi kuzidi kumwombea uzima na afya il kuendelea kuwafikia wahitaji zaidi na kwamba wanagusa wahitaji moyo wa MUNGU unafurahu na ndo sababu Mbeya Mjini inazidi kustawi.
“Mbeya mjini inastawi kwasababu ina mbolea haya mambo tunayoyafanya kusaidia watu wenye uhitaji ni kuonyesha kuwa Mbeya inastawi na itaendelea kustawi tumesema mambo ya kisiasa ni ya muhimu kwasababu wengine wanatumia Matukio haya tunayoyafanya kwa sura tofauti na hawa tuliowasaidia wapo wawili hapa kweli ndo tuseme tunataka kura”amesisitiza Dkt .Tulia.
Aidha Dkt.Tulia amesema kwamba hata akistaafu kazi hiyo ya kusaidia kujenga nyumba za wahitaji ataendelea kuzifanya na itakuwa ya kudumu kwasababu kuna watu hawasomi maandiko Biblia imewatambua maskini na watakuwepo siku zote.
Hata hivyo amesema kuwa haitakiwi kubeza juhudi za kusaidia maskini wanafikiri kuwa miundombinu ikitengenezwa kila mtu atakuwa sawa, shule zikijengwa kila mtu atakuwa sawa hata yeye wapo aliosoma nao hawajafika hapo alipo yeye .
“Kwa hiyo isifike mahali ukafikiri kuna jambo dogo la kumsaidia muhitaji ukafikiri tutafika mahali tusiwe na wahitaji kwasababu hiyo nikuombe na wewe usaidie wenye uhitaji,kwa hiyo kama unahisi hizi nyumba zinatupwa kura tushapata karibu nawe usaidie”amesema Dkt.Tulia.
Joshua Edward ni Ofisa habari na mawasiliano wa Taasisi ya Tulia Trust amesema kuwa mpaka Sasa taasisi hiyo imekabidhi nyumba tisa kwa watu wenye uhitaji na wazee wasiojiweza mkoani Mbeya.
Rocket Mwashinga ni Chifu mkuu wa mkoa wa Mbeya,amesema kwamba mambo anayofanya Spika wa Bunge Dkt.Tulia ni kwamba anagusa kila kona ikiwemo Barabara,Elimu,Bajaji, Bodaboda na kwamba unaweza ukawa Mbunge na usifanye yote hayo na kusema machifu wa mkoa wa Mbeya wanazidi kumwombea kwa yote .
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best