Na Mwandishi Wetu,TimesmajiraOnline,Pangani
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Mji Korogwe Ali Mkwavingwa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Mkoa wa Tanga baada ya kumshinda Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Seleboss.
Uchaguzi huo ulifanyika Februari 23, 2026 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, ambapo Katibu Tawala Msaidizi (Usimamizi wa Rasilimali Watu), Sebastian Masanja, alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Rashid Mchatta.
Akitangaza matokeo hayo, Masanja alisema Mkwavingwa alipata kura 28, huku Seleboss akiambulia kura 12.
Akizungumza mara baada ya ushindi huo, Mkwavingwa ameahidi kudumisha amani , umoja na mshikamano. Lakini pia ameahidi kuitengeneza ALAT Mkoa wa Tanga kuwa na uwekezaji wa miradi mbalimbali ili iweze kujiendesha kiuchumi.
“Naahidi kudumisha amani, mshikamano na umoja katika kuwatumikia wananchi. Lakini pia dhamira yangu ni kuona ALAT inasonga mbele ikiwa na miradi ya uwekezaji ili iweze kujiendesha kiuchumi” alisema Mkwavingwa.

More Stories
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina
Kihongosi: Msigombane kwa itikadi za vyama