Na Esther Macha,Timesmajira Online, Mbeya
MKAZI wa Makondeko mkoani Mbeya ,Warren Mwinuka (20)anashiliwa na jeshi la polisi mkoani hapa kwa kujifanya mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera na kutumia akaunti ya mtandao wa kijamii kwa jina la “Juma Homera”.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya ,Ulrich Matei amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Juni 7 mwaka huu majira ya saa 8.00 mchana huko maeneo ya Mama John Jijini hapa.
Aidha Kamanda Matei amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia akaunti hiyo kuwahadaa watu kwa kujifanya ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Matei amesema kuwa mtuhumiwa huyo kwa kutumia jina la mkuu wa mkoa wa Mbeya aliweza kutoa namba yake ya simu ili wananchi waweze kutoa na kupeleka kero zao mbalimbali kwake.
Hata hivyo Matei amesema kuwa upelelezi wa shauri hilo unaendelea na mara baada ya kukamilika atafikishwa mahakamani.


More Stories
Kanisa la Shincheonji la Yesu nchini Ufaransa lakanusha ripoti ya Le Parisie
Vyombo vya ulinzi na usalama Mbeya,Benki kuu kushirikiana kutatua changamoto za utapeli mtandaoni
Polisi Mbeya kuimarisha ulinzi kuelekea sikukuu ya Pasaka