November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkurugenzi wa Uvuvi atumbuliwa

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega ameelekeza kuondolewa katika nafasi yake Kaimu Mkurugenzi wa Uvuvi, Bw. Stephen Lukanga baada ya kushindwa kupanga na kutekeleza mikakati thabiti ya kukomesha uvuvi haramu nchini.

Waziri Ulega ametoa maamuzi hayo wakati akikabidhi boti (11) zenye thamani ya Shilingi ya Bilioni 1. 85 zilizotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kwa mkopo kwa wavuvi wa Mkoa wa Dar es Salaam leo Novemba 28, 2023.

Waziri Ulega amefika maamuzi hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wadau wa Uvuvi Mkoani Dar es Salaam ya kukithiri kwa vitendo vya Uvuvi haramu katika ukanda Pwani hususani Dar es Salaam.

Oktoba 4, 2023 akiwa mkoani Mwanza, katika Soko la Lumumba, Waziri Ulega alimtaka Kaimu Mkurugenzi huyo kuwa ndani ya Mwezi mmoja kuhakikisha anapanga na kutekeleza mikakati thabiti ya kukomesha uvuvi haramu nchini ambao kwa muda umekuwa ni kikwazo kwa maendeleo ya sekta ya uvuvi.

Kufuatia kushindwa kutekeleza mikakati hiyo, Waziri Ulega ameamua kumuondoa katika nafasi hiyo na kuelekeza nafasi hiyo apewe aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani, Prof. Mohamed Sheikh.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akiongea na wadau wa uvuvi pamoja na wananchi waliojitokeza katika tukio la kukabidhi boti kwa wavuvi wa Mkoa wa Dar es Salaam leo Novemba 28, 2023.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akimkabidhi vifaa vya uvuvi mmoja wa Wanufaika wa mkopo wa boti katika tukio la kukabidhi boti kwa wavuvi wa Mkoa wa Dar es Salaam leo Novemba 28, 2023.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akikata utepe ikiwa ni ishara ya kukabidhi boti kwa wavuvi wa Dar es Salaam katika tukio la kukabidhi boti kwa wavuvi wa Mkoa wa Dar es Salaam leo Novemba 28, 2023.