March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO azungumza na Wanawake Wachimbaji Katika Maonyesho ya Madini Geita

Na Joyce Kasiki,Timesmajira onlinw,Geita

MKURUGENZI  Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) CPA Venance Mwase amewapongeza wanawake wachimbaji wa madini kwa kazi kubwa na ya kuigwa wanayoifanya katika sekta ya madini, huku akiahidi kuendelea kuwashika mkono na kuwawezesha zaidi kupitia miradi mbalimbali ya shirika hilo.

Akizungumza na kikundi cha wanawake wachimbaji kutoka Chama cha Wanawake Wachimbaji Madini Tanzania (TAWOMA) waliomtembelea katika banda la STAMICO kwenye Maonyesho ya Madini ya Geita, Mkurugenzi huyo alieleza kuwa amevutiwa sana na juhudi na ubunifu wa wanawake hao.

 “Kushukuru ni jambo jema, lakini niwaambie mnafanya kazi nzuri sana. Ukiona Salma (mmoja wa wanachama wa TAWOMA) anakuja kwangu, inakata jambo na anatoka na kitu  jua nahamasishwa na mnachokifanya,” alisema Mkurugenzi huyo kwa furaha.

Amesisitiza kuwa Serikali ina dhamira ya dhati ya kuwawezesha wachimbaji wadogo, hususan wanawake na vijana, na kwamba STAMICO ipo tayari kuhakikisha inawaunga mkono kwa vitendo.

“Ahadi yangu kwenu ni kuendelea kuwashika mkono kwa sababu hamjawahi kuniangusha. Kila kidogo ambacho Serikali inatoa kupitia STAMICO, mafanikio yake tunayaona. Kwa hiyo kwa nini msipewe kikubwa?” alihoji kwa msisitizo.

Katika hatua ya kuwainua zaidi wanawake hao, Mkurugenzi huyo aliahidi kusaidia upatikanaji wa pampu za maji kwa vikundi vya wanawake wachimbaji, akisema tayari ameahidi kibinafsi kufanikisha hilo.

 “Kamilisheni ule utafiti wa kubaini mahitaji halisi ya pampu za maji. Tutaanza kutoa msaada huo kwa awamu hadi kila kikundi cha wanawake kiondokane na changamoto hiyo,” alieleza.

Akizungumzia kuhusu vifaa vya uchimbaji, alieleza kuwa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha rig moja ya kisasa inatolewa kwa wanawake tayari linatekelezwa. 

Vifaa vipo katika hatua za mwisho kukamilika na STAMICO inaendelea na taratibu za kukabidhi rig hiyo .

 “Mimi nitajua shed itakwenda wapi, na nitahakikisha vijana wanapewa mafunzo ili wakasaidie kikundi baada ya kikundi,” amesema.

Kwa upande wao, viongozi wa TAWOMA walimshukuru Mkurugenzi wa STAMICO kwa namna ambavyo amekuwa mstari wa mbele kusaidia wanawake wachimbaji, hasa katika Mkoa wa Geita ambao wamesema ndiyo mkoa uliopokea msaada mkubwa kupitia mradi wa ‘Malika wa Madini’.

Katibu wa TAWOMA Taifa Salma Ernest alieleza kuwa msaada wa STAMICO umekuwa wa hali ya juu, ikiwemo kufadhili tafiti, kutoa elimu kwa wachimbaji zaidi ya 640 na kuhakikisha vifaa vinawafikia walengwa.

 “Mapendekezo yetu kwa Mkurugenzi yalizingatiwa, na zaidi ya hapo akaongeza kipengele cha nini kifanyike kutokana na matokeo ya utafiti. Vikundi vingi vimehamasika kujiunga, na tumefikia asilimia 30 ya utekelezaji huo,” alisema Katibu huyo.

Aidha, wanawake hao walieleza kufurahishwa na ushiriki wao katika maonyesho hayo, wakisema umewapa fursa ya kutambulika, kujifunza, na kuunganishwa na taasisi za kifedha pamoja na wadau wa maendeleo.

 “Ukituletea hapa, na sisi tunajiongeza. Tumetembelea mabanda yote, tumetambulika sisi ni nani na tunafanya nini. Tumeonana na mabenki makubwa na makampuni mbalimbali – yote hayo ni mafanikio makubwa,” alieleza mmoja wa viongozi wa TAWOMA kwa shukrani.

Mwenyekiti wa TAWOMA Mkoa wa Geita Evelyne Cleophace  naye aliongeza kuwa Mkurugenzi huyo amekuwa “kama baba bora” kwa wanawake wachimbaji, ambaye amekuwa akisikiliza changamoto zao na kuwatafutia suluhisho kwa  ya Madini Geita mwaka huu yameendelea kuwa jukwaa muhimu kwa wachimbaji wadogo, hasa wanawake, kuonyesha mafanikio yao, kujifunza teknolojia mpya na kupata fursa za maendeleo kupitia mashirikiano na taasisi kama STAMICO.