December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkurugenzi 3M Network, awahimiza wanawake kujitambua kufikia ndoto zao

Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza

Wito umetolewa Kwa wanawake kujitambua,kuthubutu na kuamka ili waweze kufanya ndoto zao.

Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi wa taasisi ya 3M Network Group 2012, Betty Kwibisa,katika gala la usiku wa wanandoa(Couple’s night gala regular), ilioandaliwa na taasisi hiyo iliofanyika jijini Mwanza.

Kwibisa ameeleza kuwa, changamoto ni kuwa wanawake wengi hawajitambui na hawafahamu ni kwa namna gani wanaweza kufikia ndoto zao kutokana na kukatishwa tamaa.

“Amka nenda kwenye ndoto yako,angalie wewe unaweza unajua sisi tunapenda sana kukatishana tamaa utakuta kila mwanamke ana ndoto zake anashindwa ni namna gani ataifikia,sisi 3M Network kama mtu ana wazo lake tunalichukua na kuliweka katika uhalisia na kumuwezesha kufanya tumejikita katika kutengeneza ndoto za watu walizo nazo ili waweze kupiga hatua,”ameeleza Kwibisa.

Akizungumzia usiku huo wa wanandoa, ameeleza lengo ni kukutana na kuelimisha na kukumbusha ili kuwe na jamii yenye maadili mema na familia salama ambayo yenye uchumi wa kujitegemea.

Ameeleza kuwa zoezi hilo ni endelevu wamelianza tangu 2012 na wanatamani wapanue wigo zaidi hadi vijijini kuelimisha na kumsaidia miradi mbalimbali kwani watu wengi wamesahau vijijini kama kuna matatizo tumejikita sana mijini.

3M Network wamepanga ziara ya kwenda mpaka vijijini lengo kila familia iweze kujikwanua,wakifanya hivyo wanaamini watakuwa na jamii bora na nchi ambayo inaweza kujikwanua kiuchumi.

“Lengo ni kuelimisha jamii kuanzia ngazi ya familia ili iweze kujitegemea kiuchumi ikiwemo mahitaji muhimu, mahusiano na ndoa zimekuwa na changamoto sana tumeona mtu anaua mke wake mara hivi mara vile visa ndani ya jamii vimekuwa vingi yani tunatamani 3M network tuendelee kutoa mafunzo,”ameeleza.

Pia ameeleza kuwa ili kukabiliana na vitendo viuovu jamii inapaswa kuwa na hofu ya Mungu ili kutatua changamoto katika mahusiano.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa M-E computer software Ltd Lilian Mwakitwange, ameeleza kuwa,kupitia usiku huo wamejifunza mambo mengi.

“Tumekumbushwa wajibu wetu tunajisahau kwa sababu ya kazi na kuhangaika na maisha tunajisahau tunapopata matukio kama haya yanaturudisha kwenye mstari,tunajua hapa nakosea hapa niweke sawa,”ameeleza Mwakitwange.

Huku akiwataka wanawake wenzie wasikate tamaa kwani wananafasi kubwa katika kuhakikisha familia inakuwa bora na salama kuanzia kwa mme hadi watoto.

Mkurugenzi wa taasisi ya 3M Network Group 2012, Betty Kwibisa, akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa gala la usiku wa wanandoa(Couple’s night gala regular), ilioandaliwa na taasisi hiyo iliofanyika jijini Mwanza.(Picha na Judith Ferdinand)
Mkurugenzi wa M-E computer software Ltd Lilian Mwakitwange akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa gala la usiku wa wanandoa(Couple’s night gala regular), ilioandaliwa na taasisi ya 3M Network Group 2012 iliofanyika jijini Mwanza.(Picha na Judith Ferdinand)
Mkurugenzi wa taasisi ya 3M Network Group 2012, Betty Kwibisa akishikana mkono na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi,ambaye alikuwa mgeni rasmi katika gala la usiku wa wanandoa(Couple’s night gala regular), ilioandaliwa na taasisi hiyo iliofanyika jijini Mwanza.(Picha na Judith Ferdinand)
Baadhi ya watu waliohudhuria kwenye gala la usiku wa wanandoa(Couple’s night gala regular), ilioandaliwa na taasisi ya 3M Network Group 2012 iliofanyika jijini Mwanza.(Picha na Judith Ferdinand)