January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa aridhishwa na hatua ujenzi hospitali ya Wilaya

Na Ashura Jumapili, Timesmajira Online,Bukoba,

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2023, Abdallah Kaim,ameridhishwa na hatua mbalimbali za ujenzi wa majengo ya hospitali ya Wilaya ya Manispaa Bukoba wenye thamani ya zaidi ya bilioni 1.

Kaim, amesema hayo wakati wa kuweka jiwe la msingi wodi ya wazazi,wanawake,wanaume na jengo la kufulia katika hospitali hiyo.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka huu Abdallah Kaim ,akiongea na wananchi hospitali ya Wilaya katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba hawapo pichani

” Mwenge wa Uhuru umezindua majengo hayo baada ya kujiridhisha na hatua mbalimbali za ujenzi huo ikiwemo kupitia nyaraka mbalimbali zilizowasilishwa,”amesema Kaim.

Amesema licha ya jitihada nzuri zilizofanywa katika ujenzi huo pia mwenge umebaini mapungufu madogo madogo ambayo ametoa maelekezo kufanyiwa marekebisha ndani ya siku tatu na kuwasilisha taarifa kwake.

Katika hatua nyinge kiongozi huyo amegawa vyandarua kwa baadhi ya wananchi na kuwataka kuvitumia kama ilivyokusudia na Serikali ili kuepuka ugonjwa wa maralia.

“Msivitumie vyandarua hivi katika shughuli za kilimo,uvuvi na matumizi mengine yasiyo sahihi,”amesema.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa kiongozi huyo jengo la wazazi limetumia kiasi cha milioni 485.3,wodi ya wanawake milioni 180. 9,wanaume milioni 129.8 na milioni 202.2 huku
kiasi kilichosalia kwenye akaunti benki ni milioni 1.7.

Ambapo Ujenzi wa majengo hayo na mengine yaliyokwisha kujengwa yatakuwa na faida kwa wananchi wote wa Manispaa hiyo ambapo zaidi ya watu milioni 1,wakiwemo wagonjwa watakaopatiwa rufaa kutoka vituo vyote 32 vya kutolea huduma ya afya vilivyopo ndani na nje ya Manispaa.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru akipima katika moja ya majengo ya hospitali ya Wilaya katika Halmashauri ya Manispaa Bukoba

Aidha baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa wakimbiza mwenge kitaifa , Mhandisi wa ujenzi Manispaa ya Bukoba Joshua Ntinge amesema ameyapokea na anayafanyia kazi.