January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkenda: Ubora wa elimu siyo kuboresha mitaala tu, walimu na wakufunzi waandaliwe pia

Na Joyce Kasiki, TimesMajira Online, Dodoma

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema suala la ubora wa elimu siyo suala la mitaala peke yake  bali suala hilo linapaswa liende sambamba na kuwaandaa vyema walimu na wakufunzi katika vyuo vya ualimu nchini.

Profesa Mkenda ameyasema hay oleo jijini Dodoma katika fupi ya kugawa kompyuta 300  ambazo ni kompyuta mpakato na kompyuta za mezani kupitia mradi wa Elimu ya Ualimu (TESP) unaofadhiliwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Serikali ya Canada kupitia Ubalozi wake hapa nchini.

“Suala la  walimu na wakufunzi ni suala muhimu ,tunapokuwa na mitaala mizuri walimu hawatoshi haisadii.”amesema Profesa Mkenda na kuongeza kuwa

“Hatuwezi kuwa na sehemu ambazo walimu hawatoshi halafu tukadhani kwamba tukibadilisha mitaala itatusaidia,lazima kuwepo na walimu wa kutosha kufanyia kazi ile mitaala…, na taratibu za ufundishaji sasa hivi zinahitaji walimu na darasa dogo zaidi ili kuwashirikisha wanafunzi kwa sababu mwelekeo ni kuhakikisha unawashirikisha wanafunzi  zaidi .”

Aidha amesema,seriali inatarajia kuanza utekelezaji wa kubadilisha sera ya elimu ambayo moja kwa moja itaenda kubadilisha na mitaala huku akisema licha ya  kazi hiyomkuwa na gharama kubwa lakini kazi hiyo inakwenda kuanza mara moja.

“Hili suala litakuwa shirikishi maana  hatutaki kuwa na mabadiliko ya mara kwa mara kwenye elimu hivyo tunataka mitaala iwe mizuri.”amesisitiza

Vile vile amesema kuwa Miundombinu na vitndea kazi vya walimu ni muhimu ikiwa ni pamoja na kuwa na vitabu vya kiada na ziada.

Akizungumzia kuhusu zoezi hilo la ugawaji kompyuta kwa vyuo vya ualimu Profesa Mkenda amesema,zoezi hilo ni mwelezo ambapo amesema,tayari Wizara yake imeshatoa mafunzo ya tehama katika kufundisha na kujifunzia kwa wakufunzi wote 2,300 kutoka vyuo vya ualimu vya serikali ambayo idadi ni 35.

Pia mesema,Wizara hiyo imeshagawa vifaa vya tehama zikiwemo kompyuta za mezani 1,120,kompyuta mpakato 113 na projekta 186 kwenye vyuo hivyo.

“Vifaa hivi leo ni  nyohgeza ili kukidhi mahitaji hii itasaidia kupungzua matumizi ya uwiano wa kompyuta kwa wananchuo kutoka kwa wanachuo 28 kwa kompyuta moja hadi wanachuo wawili kwa kompyuta moja…,na huko mbele tunataka kila mwanachuo atumie  kompyuta yake.”amesema na kuongeza kuwa

“Hii inatuhakikishia ukufunzi unaotolewa katika vyuo vyetu utamfikia mwanachuo vizuri na kumuandaa kwa ajili kwenda kutusaidia kufundisha vijana wetu.”

Aidha amesema,kwa matumizi ya vifaa na mifumo  ya tehama iliyoboreshwa kwenda vizuri inahitaji pia kuwepo kwa mitandao imara .

Kufuatia hali hiyo Waziri huyo amesema Wizara itaviunganisha vyuo vyote vya ualimu na mkongo wa Taifa ili kuhakikisha kuwa vyuo vinaweza kupata mtandao imara utakowezesha wakufunzi na wanachuo kutumia ufundishaji na ujifunzaji kwa ufanisi.

Amesema,kwa mwaka huu wanatarajia  kuungansha vyuo 15 vya ualimu katika mkongo huo na kazi hiyo imeshaanza.

Amewataka wakuu wa vyuo hivyo nchini kuhakikisha kompyuta hizo zinatumika kwa matumizi yaliyokusudiwa na siyo vinginevyo lakini pia kuhakikisha zinatunzwa vizuri.

Kwa upande wake Niabu wa Wizara hiyo Omary Kipanga amesema ,kupitia mtradi huo   kazi kubwa imefanyika ikiwemo  katika eneo la maabara za Tehama pamoja na vifaa vya Tehama.

“Kama tunataka  kufanya mapinduzi na magezui katika ufundishaji wa elimu kwenye Tehama tayari tupo vizuri ,miundombinu ipo kwa ajili ya walimu wetu kuhakikisha pale tunapotaka  kwenda tunaweza kufika.”Amesema Kipanga

Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Caroline Nombo amesema ,shughuli za kuendeleza mradi wa kuendeleza elimu ya ualimu

Mradi unatekelezwa kwa ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na serikali ya Canada kupitia ubalozi wake hapa nchini.

Amesema,mchango wa serikali katika mradi huu ni dola za Canada milioni 53  huku mchango wa serikali ya Tanzania ukiwa ni  katika kugharamia shughuli mbalimbali za uendeshwaji wa vyuo zikiwemo gharama za malipo ya chakula kwa wanachuo na gharama za mafunzo kwa vitendo.

Aidha amesema,dhumuni la mradi huo unaotarajia kukamilika  katika mwaka wa fedha wa 2023/24 ni kuendeleza elimu ya ualimu hapa nchini kwa kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kupitia masuala uboreshaji wa miundombinu ya utoaji wa mafunzo ya ualimu katika vyuo vyote vya serikali.

Vile vile ametaja dhumuni linguine kuwa ni kutoa vifaa vya kufundishia na kujifunzia,kuimarisha mifumo ya miundombinu ya tehama na kuwaendeleza kitaalam na kuwajengea uwezo watendaji katika utoaji wa elimu ya ualimu nchini .