May 15, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mke wa Rais wa Finland atembelea Makumbusho ya Taifa

Na Mwandishi wetu,TimesmajiraOnline,Dar

MKE wa Rais wa Jamhuri ya Finland Suzanne Innes ametembelea Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam na kufurahishwa na uhifadhi wa urithi wa asili na wa utamaduni ikiwemo fuvu halisi la mwanadamu wa kale (Zinjanthropus).

Ziara hiyo fupi iliyofanyika katika Makumbusho hayo mapema leo Mei 14, 2025 Innes aliogozwa na mwenyeji wake Katibu Mkuu Wizara ya Maliasiri na utalii , Dkt Hassan Abbas ambapo aliweza  kujionea maeneo mbalimbali ikiwemo eneo ambalo limeifadhi historia kubwa ya nchi ya Tanzania

Moja ya maeneo aliyotembelea ni pamoja na kuona Utamaduni wa kitanzania, historia ya mwanadamu,pamoja na kufuraishwa na fuvu halisi la mwanadamu wa kale

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa ziara hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Maliasiri na Utalii Dkt Hassan Abbas amesema  wizara ya Maliasiri na utalii imekuwa na ushirikiano  mkubwa na wa muda mrefu na Serikali ya Finland  hasa katika sekta ya misitu na maeneo ya kubadilishana wataalamu wa misitu

“Sisi na Finland ni ndugu kabisa hata ukitembelea katika makumbusho yetu utaona picha ya hayati baba wa Taifa mwalimu Nyerere mwaka 1973 kati moja ya ziara zake alikwenda Finland”amesema Dkt Abbas

Pia amesema katika sekta ya misitu Serikali ya Finland na  Tanzania zimekuwa na ushirikiano wa zaidi ya miaka 40 ambapo wamekuwa  wakisaidiana katika ngazi za utaalamu .

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa  makumbusho ya Taifa ,Noel Lwoga amesema kutembelewa na mke wa Rais wa Finland katika makumbusho hiyo kumeweka  alama kubwa ya mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita katika kuutagaza utalii .

Pia amesema ni alama ya mafanikio ya wizara ya Maliasiri na utalii katika kupanua wigo wa vivutio vya utalii .

“Tulizoea labda wageni wageweza  kwenda mbuga za wanyama sasa wanafika katika makumbusho ni uwekezaji mkubwa ambao wizara na Serikali ya awamu ya sita imefanya katika kufungua mazao ya utalii wa Mali kale “amesema

Mkurugenzi Mkuu huyo alitumia fursa hiyo kuwaomba  watanzania  na wageni kutoka nje ya Nchi kuendelea kutembelea makumbusho za taifa kwa ajili ya kujifunza historia na urithi wa Taifa kufahamu utamaduni na mwingiliano wa Taifa na mataifa mengine.