March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkazi wa Mwanga ajishindia Mil. 5/=

Na Mwamdishi Wetu, Timesmajira Online

KAMPUNI ya Mawasiliano Tanzania, Yas jana imekabidhi hundi ya shilingi milioni tano (5) kwa Petro Mefurda, mkazi wa Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Mefurda ameibuka mshindi wa droo ya tatu ya kampeni inayoendelea ya Tunasheherekea Pamoja na Mwaka mmoja wa Yas.

Akizungumza wakati wa makabidhiano yaliyofanyika mjini Moshi, Meneja wa Duka la Yas Moshi, Francis Joseph amesema hatua hiyo ni sehemu ya dhamira ya kampuni kuwashukuru wateja wake kwa kuendelea kuichagua Yas katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kubadilika kwa chapa.

Joseph amebainisha kuwa, kampeni ya Tunasheherekea Pamoja na Mwaka Mmoja wa Yas imebuniwa kuleta fursa kwa watumiaji wa huduma za Yas kujishindia zawadi mbalimbali zenye lengo la kuongeza thamani katika maisha yao.

“Tunatambua mchango wa wateja wetu katika safari ya Yas. Ndiyo maana tunawazadia wateja wetu kwa namna itakayowawezesha kwenye shughuli zao mbalimbali,” alisema.

Kwa upande wake, mshindi Petro Mefurda, ameelezea namna anavyopanga kutumia zawadi hiyo ya Shilingi Milioni 5, alisema ushindi huo umekuja katika kipindi sahihi na utasaidia kuongeza mtaji ili kuboresha shughuli zake za kijamii na kiuchumi.

“Sikutarajia kabisa, lakini Yas wamethibitisha kuwa Kampeni zao ni halali na zenye manufaa kwa jamii.

“Nawashauri wateja wa Yas kuendelea kushiriki ili nao waweze kushinda,” amesema Mefurda.

Kampeni ya Tunasheherekea Pamoja inaendelea kote nchini na wateja wote wa Yas wanahimizwa kuendelea kutumia huduma za kampuni hiyo.

Lengo likiwa kujipatia nafasi ya kushinda zawadi za kila siku, wiki, pamoja na zawadi kuu ya milioni 100 mwishoni mwa kampen.