Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
MKAZI wa Bunju jijini Dar es Salaam, Bw. Yusuph Constantine Muhoja ameibuka mshindi wa jumla wa milioni 50 kwenye Kampeni ya mwisho wa mwaka ya Magift ya Mixx Pesa kutoka Mixx.
Hafla ya kufunga kampeni hiyo, imehudhuriwa na viongozi waandamizi wa Yas na Mixx akiwemo Afisa Mtendaji Mkuu wa Yas, Bw. Pierre Canton Bacara na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx, Angelica Pesha, wateja na wadau wa kibiashara wa Yas na Mixx.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi hiyo kwa mshindi wa jumla wa Kampeni hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx, Angelica Pesha, amesema Kampeni ya ‘Magifti ya Mixx Pesa’ imegusa maisha ya watanzania kwa namna ya kipekee.
Tumewaona kina mama wakilipa ada za watoto, vijana wakikuza biashara zao, na familia zaidi ya 40 zikianza mwaka mpya kwa matumaini mapya. Hii ndiyo maana ya kuwa mshirika halisi wa kifedha kwa watanzania,” amesema.
Kupitia kampeni hii, Mixx imeweza kuibua zaidi ya Ma-Mixxionea 44 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania, wakiwemo.

Washindi 37 wa TSh 1 milioni, Washindi 5 wa TSh 5 milioni, Mshindi 1 wa TSh 10 milioni Na mshindi mkuu wa TSh 50 milioni, Yusuph Constantine Muhoja.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Biashara Mixx, James Sumari, alisisitiza dhamira ya Mixx ya kutimiza ahadi zake.
“Leo tunafunga kampeni yetu ya Magift ya Mixx Pesa, lakini hatufungi safari ya Mixx.
“Kampeni hii imekua sehemu kubwa ya ahadi yetu ya kuwa mshirika wa karibu wa kifedha kwa kila Mtanzania – kupitia huduma za malipo, mikopo, akiba, na huduma nyingine za kidijitali.
“Tumeshuhudia zawadi zikibadilisha maisha ya watanzania. Tunajua fedha tulizokabidhi, zitafungua milango mipya ya mafanikio, na tunajivunia kuwa sehemu ya safari hiyo,” amesema.

More Stories
TFF yatinga na safu tatu mpya
Mkazi Kisarawe ashinda Mil. 100, Kampeni ya ‘Tunasherehekea Pamoja’
Ajinyakulia Mil. 5/- Kampeni ya Yas ‘tunasherehekea mwaka mmoja’