Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
MKAZI wa Kisarawe, Veronica Kilango ameshinda zawadi kuu Kampeni ya shilingi milioni 100.
Kupitia Kampeni ya ‘Tunasheherekea Pamoja – Mwaka Mmoja wa Yas’, mshindi huyo amekabidhiwa zawadi yake leo kupitia hafla iliyofanyika wilayani Kisarawe akiibuka mshindi wa jumla.
Kampeni hiyo iliyodumu kwa takriban mwezi mmoja imekuwa na lengo la kuwazawadia wateja wa Yas kwa kuipokea chapa hiyo kwa mikono miwili tangu kufanyika kwa mabadiliko ya chapa mwishoni mwa mwaka 2024.
Vilevile ni dhamira ya Kampuni ya Mawasiliano ya Yas, kuendelea kuwawezesha watanzania kupitia huduma za kidijitali zenye kasi na kuaminika kupitia zawadi za vifaa mbalimbali vya kielektroniki kama Simu na Router za 5G.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi wa Kanda ya Pwani Kusini, Fadhila Saidi, alibainisha kuwa kampeni hiyo imefanikiwa kuwazawadia watanzania zaidi ya 110 kote nchini.
Amesisitiza kuwa, Kampeni ilikuwa na ushiriki mkubwa kutoka kwa watanzania ikionesha imani ambayo wananchi wanayo kwa chapa ya Yas.
“Kati ya mwezi uliopita, tumeshuhudia ari kubwa na ushiriki wa wateja wetu.
“Kampeni hii inaakisi ahadi ya chapa yetu – siyo tu kuwa mtoa huduma wa mawasiliano, bali kuwa mshirika sahihi katika ndoto na maendeleo ya Watanzania.” Amesema.
Aliongeza kuwa, Kampeni ilikua na zawadi mbalimbali ikiwemo shilingi milioni 1 za kila siku, Shilingi milioni 5 za kila wiki, safari ya Dubai kwa washindi 10 iliyolipiwa kila kitu, vifaa mbalimbali vya kidijitali kama simu za mkononi na routers za 5G na zawadi kuu Kampeni ya shilingi milioni 100 mwishoni mwa Kampeni.

Kwa upande wa mshindi mara baada ya kupokea zawadi yake, Kilango ameeleza shukrani zake za dhati kwa Yas na kusema ushindi huo utambadilishia maisha yake.
“Bado siamini kwamba mimi ndiye mshindi wa milioni 100. Kwa hakika, namshukuru Mungu. Pia naishukuru Yas kwa kunitambua, na ninaona hii kama zawadi kutoka kwa Mungu.
“Nimepanga kutumia sehemu ya pesa hizi kuwekeza, kukuza biashara yangu ndogo, na kusaidia kituo changu cha watoto yatima, kwani ninaishi na watoto yatima nyumbani.” ameaema.
Nae Mteja wa Yas na mkazi wa Kisarawe mkoani Pwani, Saidi Ally Njame ameeleza hisia zake juu ya kuupenda mtandao wa Yas kwani umekua mtandao unaofanya mambo yake kwa uwazi na kujali jamii.
Ameeleza kuwa, ameshuhudia mteja mwenzake wa Yas mkazi wa Kisarawe, Veronica Kilango akikabidhiwa zawadi yake ya milioni mia moja baada kuibuka mshindi wa kampeni ya tunasherehekea mwaka mmoja.

Jambo hilo limempa morali wa kuendelea kutumia huduma za Yas akiamini siku moja nae anaweza kuibuka mshindi katika kampeni zijazoTukiangalia mbele.
Yas imeeleza dhamira yake ya kuendeleza uwekezaji katika upanuzi wa mtandao, ubunifu wa kidijitali, na suluhisho za teknolojia ya kifedha.
Kampuni pia ilisisitiza msaada wake kwa jitihada za taifa katika mabadiliko ya kidijitali, hasa katika kurahisisha biashara, kilimo, elimu, na ujasiriamali kote nchini.
Kampeni hiyo haijaimarisha tu uhusiano wa Yas na wateja wake bali pia ilithibitisha nafasi yake kama mshirika sahihi wa kidijitali anayeaminika kwa watanzania.

More Stories
TFF yatinga na safu tatu mpya
Ajinyakulia Mil. 5/- Kampeni ya Yas ‘tunasherehekea mwaka mmoja’
Mkutano Mkuu TFF kufanyika Februari 28,2026