November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mizani ni vipimio halali masokoni

Mfanyabiashara aliyefahamika Small kamata akipima nyanya ziliko katika kisado na kuzipima katika mzani

Na Bakari Lulela, Timesmajira Online DSM

WAKALA wa vipimo WMA mkoa wa kinondoni wamesema bidhaa zilizo halali sokoni haziendi sawa na bei halisi ya bidhaa kwa wateja.

Akizungumza jijini kuelekea katika maadhimisho ya siku ya vipimo duniani ambayo hufanyika kila mei 20 kila mwaka meneja wa WAKALA hao, Lilian Mwombeki amesema bidhaa zinazopimwa ikiwemo nyanya, vitunguu vilivyo kwenye visado huwa havilingani na bei halisi inayouzwa kweye mizani.

“WAKALA wa vipimo tunazingatia Sheria ambapo wafanyabiashara wanatakiwa kuuza bidhaa kwa bei ambazo ni sawa na vipimo (vifungashio) ama mizani maalumu,” amesema Mwombeki

Aidha, Mwombeki amesema WAKALA hao hufanya kaguzi za kustukiza kila mara lakini hufanya zoezi la kuhakiki mara moja kwa mwaka pia huwapa elimu wateja hao.

Hata hivyo meneja huyo amesema kutokana na Sheria zao kukiukwa huwachukulia hatua na kuwalipisha faini wale wote wanaokiuka maagizo, kauli mbiu ya mwaka huu inasema tunapima Leo kwa kesho endelevu ambapo inataka wafanyabiashara kufanya shughulu zao kwa uadilifu.

Moja wa wafanyabiashara katika soko la magomeni Dar es salaam Small kamata amesema wao hufanya biashara kwa lengo la kupata faida lakini amedai kuwa bidhaa zake ni rafiki kwa walaji wanaopata mahitaji kwake.

Mfanyabiashara huyo amedai kuwa huuza mazao ya nyanya kwa wastani wa kilo 3 shilingi elfu 7 na sado 1 shilingi elfu 7 ambapo kwa viwango vya wakala inakuwa haiendani kwa utofauti wa gramu 150 ambapo ni hasara kwa wateja.

Pia akieleza kwa upande wa bidhaa za vitunguu na viazi mviringo hutumia mizani na visado kama kipimio kwa wateja ambapo amesema huwapatia faida ndogo kutokakana na mzunguko wa kibiashara toka kwa mkulima hadi kufika sokoni.

Meneja wa WAKALA wa vipimo WMA mkoa wa kinondoni Dar es salaam Lilian Mwombeki akielezea muhimu wa vipimo vya mizani ni muhimu kwa wauzaji na wateja wao