March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mixx Yazindua Kampeni ya ‘Kila Hatua Mixx’ mkoani Tanga

Na Mwandishi Wetu,Timesmajira

MIXX, Kampuni ya huduma za kifedha nchini Tanzania, imeendeleza kampeni yake ya ‘Kila Hatua Mixx’ katika mkoa wa Tanga.

Hatua hiyo inalenga kuongeza ujumuishwaji wa kifedha na kukuza uchumi wa kidigitali miongoni mwa wakazi wa Kanda ya Pwani Kaskazini.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Amani Sailoja, Kaimu Mkurugenzi wa Yas – Kanda ya Pwani ya Kaskazini, alisema
Safari ya Mixx ilianza mwaka 2010 kwa ndoto ya kuhakikisha kila Mtanzania anapata fursa ya kushiriki kikamilifu katika huduma za kifedha.

” Miaka 15 baadaye, zaidi ya milioni 20 wanatumia Mixx kila mwezi kufanya miamala yenye thamani ya takribani shilingi trilioni 6,” alisema Sailoja.

Alisema, Mixx ni jukwaa lenye nguvu katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa kidigitali nchini, likiwa na mafanikio yafuatayo:

“Ajira zisizo za moja kwa moja kwa maelfu ya vijana kupitia mtandao wa mawakala zaidi ya 200,000.

“Wafanyabiashara zaidi ya 500,000 wanapokea malipo salama kidigitali.

“Zaidi ya taasisi na makampuni 3,000 hutumia Mixx kwa malipo makubwa na makusanyo ya kifedha.

“Wateja milioni 6 wamepata mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 1.

“Zaidi ya shilingi bilioni 600 zimewekwa akiba, ikithibitisha utamaduni wa kuweka akiba kwa wananchi”.

Hata hivyo alisisitiza umuhimu wa mkoa wa Tanga, kuwa ni kitovu cha kilimo, biashara ndogo na za kati, na wajasiriamali wengi wanaochangia uchumi wa kanda.

Aidha, alisema Uzinduzi wa kampeni ya Kila Hatua Mixx unalenga kuchochea huduma salama, haraka na za kidijitali zinazowawezesha kushiriki kikamilifu katika uchumi.

“Kampeni ya Kila Hatua Mixx inalenga kuchochea ujumuishwaji wa kifedha hasa kwa vijana, wanawake, na wajasiriamali wadogo, kupitia huduma kama Bustisha, Nivushe Plus, Kibubu, na Lipa kwa Simu.

” Mixx inaendelea kuwa rafiki na mshirika wa kifedha kwa kila mwana Tanga, ikichangia moja kwa moja ukuaji wa uchumi wa kanda na taifa.

Sailoja aliwashukuru wadau wote wa Kanda hiyo, ikiwemo Tanga na Morogoro, kwa kuendelea kutuamini na kutumia huduma za Mixx. Ushirikiano wenu ni msingi wa mafanikio ya kampeni yetu ya Kila Hatua Mixx. Mixx – Ni zaidi ya Pesa!”

#