Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza
Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza,imeungana na Watanzania wengine kumtakia heri ya kumbukuzi ya kuzaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kupanda miti 2,361 maeneo mbalimbali wilayani humo.
Pia ikiwa ni njia ya kumuunga mkono Dkt.Samia katika juhudi zake za kutunza na kuhifadhi mazingira,ambapo Wilaya ya Ilemela ilitumia Januari 27,2026 kupanda miti hiyo zoezi lililoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda katika ofisi za Wilaya hiyo.

Ambapo Mtanda,ametoa wito kwa wananchi kupanda miti katika makazi yao ikiwa ni sehemu ya uhifadhi wa mazingira huku akisisitiza kuwa kitendo hicho ni cha kizalendo na ni sehemu ya ibada na faida kwa vizazi vijavyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilemela,Amiri Mkalipa,amesema zoezi la upandaji miti wilayani humo limeanza mapema kwa kupanda miti ya matunda kwa ajili ya kivuli na kuhamasisha lishe bora.

Mkalipa,amesema watumishi wa Wilaya hiyo,wanamuunga mkono Rais kwa kuchapa kazi na kuhakikisha amani na usalama unakuwepo, ukusanyaji wa mapato, utatauzi wa migogoro na kuwasikiliza wananchi kila mmoja kwa nafasi yake.
“Kwa niaba ya wananchi wa Ilemela tunamtakia heri Rais Samia katika kumbukuzi ya siku yake ya kuzaliwa.Naishukuru serikali kwa kutuleta fedha nyingi zilizosaidia uboreshaji wa miundombinu na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa soko la kimataifa la samaki Kirumba na barabara zake pamoja na ujenzi wa shule za msingi,”amesema Mkalipa.




More Stories
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina