Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online
MUANDAAJI nguli wa shindano la urembo kanda ya Kilimanjaro Dotto Sang’wa ambaye pia mmiliki wa kampuni ya Dee’s Bridal, amewakaribisha wadau mbalimbali kujitokeza kudhamini shindano hilo mwaka huu.
Kilimanjaro ni moja ya mkoa unaofanya vizuri katika shindano la miss Tanzania ambapo mwaka huu taji hilo linashikiliwa na mlimbwende kutoka kanda hiyo ya Kaskazini.
Akizungumza na wandishi wa habari, Dotto amesema anakaribisha makampuni ambayo yanaweza kuungana nae kufanya shindano hilo ambalo limekua likiibua vipaji vya wasichana hapa nchini.
“Nichukue nafasi hii kuwaomba wadau na serekali kuungana nami kufanikisha mchakato wa kumpata mrembo atakaye wakilisha mkoa wetu katika shindano la taifa ambapo tunatarajia ataenda kutetea taji tunaloshikilia,” amesema Dotto.
Ameongeza kuwa, tayari mchakato wa kuwapata washiriki umeshaanza na mwishoni mwa mwezi Mei wanatarajia kufanya uzinduzi mkubwa kama ilivyo kawaida ya mkoa huo.
%%%%%%%%%%%%
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA
Coca-cola ‘Kitaa Food Fest’ yahitimishwa kwa mafanikio