January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

MISA YAWAPIGA MSASA WAANDISHI RADIO ZA KIJAMIII TANZANIA

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania,wamefanya mafunzo maalumu ya kuwajenga waandishi wa habari wa radio za kijamii kutoka mikoa mbalimbali nchini ili kuongeza uelewa kuhusu uhuru wa kujieleza.                                                             

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo,mtoa mada katika ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari, mkoa wa Arusha, Mussa Juma, alisema ni muhimu ifikiwe wakati waandishi waweze kuwa na uhuru wa kujieleza na kutoa taarifa kwa jamii pasipo kupata vitisho vyovyo vitakavyo mkwamisha katika kazi yake.

Alisema kupitia semina za utoaji elimu kwa wanahabari zinazotolewa na MISA ziwe chachu ya kuwajenga katika taaluma zao kuweza kuwajibika ipasavyo kwa kufuata sheria, taratibu na kanunu zilizo wekwa na serikali.

“Zipo sheria, sera na miongozo zinazo wawezesha wanahabari kupitia taaluma zao KUFANYA KAZI KWA uhuru kwa maslahi ya jamii kwa ujumla ijapo kuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakitumia vibaya sheria hizo kwa kufanya vitisho kwa waandishi na kufanya waandishi kushindwa kufanya kazi yao kwa ufanisi mzuri” Amebainisha Juma

Kwa upande wake mwakilishi wa kituo cha idhaa ya Kiswahili (BBC) mkoa wa Dodoma, Abubakar Famau, alisema wanahabari wana mchango mkubwa sana katika jamii kwani wamekuwa ni kiungo kikubwa baina ya serikali na wananchi hivyo jamii hususani viongozi wan chi waweze kuthamini mchango wanano utoa kwa kuwapa ushirikiano pindi wanapo kusanya taarifa kwenye taasisi hizo.

Amsema licha ya kwamba matukio mbalimbali yaliyowapata waandishi wa habari kama kifo, kupotea katika mazingira ya kutatanisha pamoja na vitisho lakini isiwe sababu ya kutofanya wajibu wako kwa jamii.

“Serikali ya awamu hii inajitahidi sana kuwaweka pamoja waandishi kwa kutizama masilahi yao na ndio maana imeweka kiwango Fulani cha elimu ambacho kitawawezesha waandishi wengi kuishi katika hali nzuri na japo yapo matukio tunayaona yanawapata waandishi lakini serikali pia inafanya kila juhudi kuimarisha sheria zitakazo mlindwa mwandishi wa habari”. amesema Famau.

Nae mshiriki kutoka kituo cha radio cha A-FM, Victor Samweli, amesema mafundisho hayo yamekuwa mwanga hususani kwa waandishi wachanga wanaotoka vyuoni na kuingia kazini na yamewafanya kutambua haki na wajibu wao katika tasnia ya habari na kuahidi kuwajibika ipasavyo kwa kufata sheria na taratibu zilizo wekwa na Serikali.

“Ni siku ya pili sasa tuko kwenye mafundisho haya yaliyoandaliwa na MISA na kwakweli kuna baadhi ya vitu tunavipata kama moja ya elimu ambayo itatusaidia sna akatika ufanisi wa kazi zetu na pia tuaiomba serikali iweze kuangalia na kuwawajibisha wale wote wanao kiuka sheria kwa kuwapa vitisho waandishi wa habari na kufanya kazi kuwa ngumu”. amesema Victor