Na Mary Margwe, TimesMajira Online, Mbulu
Jumla sh.bil.1.6 zimetumika kugharamia miradi mitano (5) iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru 2022 katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu,Mkoani Manyara,
Akizungumza wakati akipokea Mwenge wa Uhuru kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Abubakary Kuuli, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Yefred Myenzin alisema hiyo ndio miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru 2022.
Myenzi alisema mwenge wa Uhuru ulipoingia katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu, ulifanya kazi ya kuzindua miradi miwili, nankuweka jiwe la Msingi katika miradi mitatu.
” Miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru ni pamoja na mradi wa ujenzi wa miundombinu ya barabara ya lami iliyopo mtaa wa Uhuru kata ya uhuru ambao ujenzi wake unaendelea na kugharimu sh.mil.499,762,000 , fedha kutoka serikali kuu” alisema Myenzi.
Aidha miradi mingine iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru ni mradi wa vijana wa boda boda kilichopo Mbulu Mjini ambao tayari kikundi kimesajiliwa , kikundi kilipata mchango kutoka kwa wananchi sh.mil.1,843,500 pamoja na Halmashauri kukichangia sh.mil.12,985,000, mradi uliogharimu jumla ya sh.mil.14,828,500.
Aidha Myenzi alisema mradi wa Maji katika kijiji cha Qalieda ujenzi wa tanki moja la Maji unaendelea, ambapo Mwenge wa Uhuru umeupitia mradi huo na kuweka jiwe na Msingi,mradi uliogharimu jumla ya sh.mil.630,390,237.86.
” Kwenye mradi huu wa Maji serikali kuu umechangia sh.mil.630,390,237.86, pia kuna mradi wa madarasa mawili ya shule ya sekondari NOWU liyopo mtaa wa Ayamaami, mradi ambao umekamilika na Mwenge wa Uhuru umezindua madarasa hayo mawili, huku ukigharimu jumla ya sh.mil.40 fedha kutoka serikali kuu” alifafanua Myenzi.
Hata hivyo alisema katika kijiji cha Hareabi ujenzi wa kituo cha afya unaendelea nabnmwenge wa Uhuru umeupitia mradi huo na kuweka jiwe la msingi, mradi uliogharimu jumla ya sh.mil.501,800,000, huku wananchi walichangia mradi huo sh.mil.1.8 wakati serikali kuu ikichangia sh.mil.500.
Naye Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2022 Sahili Geraruma alisema watumishi na viongozi mbalimbali wamekua wakijijengea tabia ya kuwa ” Ujio wetu ni kuja kuwaumiza ama kuwaonea wakati wa ukaguzi wa miradi, sisi hatukuja huku kukataa miradi bali tumekuja kuchochea maendeleo ya miradi.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba