December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Miongozo minne yazinduliwa kuboresha elimukwa wenye mahitaji maalum

Na Joyce Kasiki,Dodoma.                     

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Tekno amezindua miongozo minne ambayo imelenga kuboresha utoaji wa Elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum.    

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa miongozo hiyo Waziri Mkenda alisema,hatua hiyo ni kufuatia maono makubwa ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kutaka kutoachwa nyuma katika suala la Elimu kwa mtoto yeyote.

Aidha Waziri Mkenda amesema lugha ya alama kwa walimu tarajali wanaopitia vyuo vya ualimu kuanzia hivi sasa itakuwa ni lazima kujifunza.

Amesema miongozo yote hiyo ni muhimu katika kutatua changamoto zinazoikabili wanafunzi wenye mahitaji maalum huku akisema matarajio ya Serikali katika miongozo hiyo ni kuleta chanya katika sekta ya Elimu hasa kwa kundi la watoto wenye mahitaji maalum.

Ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa kwa Viongozi na taasisi na wadau kuendelea kuhamasisha umuhimu wa Elimu maalum huku akiwaasa wazazi na walezi nchini wenye watoto hao waone imuhimu wa kuwaandikisha shule Ili Serikali Ione jinsi ya kuwafikia hata wakiwa nyumbani.

Akitambulisha miongozo hiyo Mkurugenzi wa Elimu Maalum Wizara ya Elimu,Sayansi na Tekno;ojia Dkt.Margareth Matonya ametaja miongozo hiyo kuwa ni Muongozo   wa shule ya nyumbani kwa watoto ambao hawawezi kukaa darasani ambao alosema  utawasaidia kuhakikisha watoto hao hawaachwi nyuma. “Muongozo huu unalenga kuwafuata  watoto majumbani na kuwafundisha masomo wanayofundishwa wengine shuleni.”

Miongozo mingine ni wa ziara ya nyumbani  ambao unaenda kuwasaidia upatikanaji wa taarifa wa akina nani wamefanyiwa ziara ya nyumbani na huu unawahusu hasa watoto wenye ulemavu wa usonji.

Pia amesema Muongozo mwingine ni wa uendeshaji Elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum ambao utasaidia kubainisha vipawa na vipaji kwa kundi la watoto hao na Mwongozo  mwingine ni wa  uanzishwaji na usimamizi wa shule ya watoto wenye mahitaji maalum nchini ambao utasaidia kutambua vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum.

Awali mzazi wa Mtoto  Ally Kinara mwenye changamoto ya magonjwa  adhimu aliishukuru Serikali kwa kuandaa na kuzindua Miongozo hiyo kwani watoto wengi walikiwa wanakosa haki muhimu ya kupata Elimu.

“Nakumbuka mwanangu Ally akiwa na miaka Saba aliona watu wakiwa wamevaa majohonna kofia,akaniuliza mama Ili na Mimi nivae hivyo natakiwa nifanye Nini,pale ndio nikaona wakati muafaka wa Ally kwenda shule umefika,lakini nilipoenda kumuandikisha shule alikataliwa kutokana na Hali yake,nililia sana,lakini sikulia kwa ajili ya Ally,nililia huku jikijiuliza ni watoto wangapi hapa nchini wanakosa hii haki,kwa niishukiuru Serikali kwa kuleta miongozo hii ambayo sasa hata watoto wenye changamoto ya magonjwa  adhimu sasa wanaenda kupata Elimu na kufikia ndoto zao.”amesema mzazi wa Ally