ATLANTA, Georgia
LICHA ya kumkosa MVP mara mbili, Giannis Antetokounmpo, Milwaukee Bucks imefanikiwa kutinga Fainali ya Ligi Kuu ya Mpira wa Kikapi nchini Marekani NBA, kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1974, baada ya kuichapa Atlanta Hawks vikapu 118-107 katika Game 6 ya fainali ya Ukanda wa Mashariki iliyochezwa Alfajiri ya leo.
Ushindi huo umetokana na mchango mkubwa wa Khris Middleton aliyeifungia timu yake pointi 32, zikiwemo pointi 16 mfululizo katika kota ya tatu iliyoamua mchezo.
Kwa matokeo hayo, Milwaukee inatinga nusu fainali kwa ushindi wa jumla wa series 4-2 na itakutana na Phoenix Suns, washindi wa ukanda wa Magharibi – Game 1 ya kwanza itakuwa Alfajiri ya Jumatano huko Phoenix.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo kocha wa Milwaukee Mike Budenholzer amesema, ni ushindi mzuri kutokana na kukiandaa vyema kikosi chake jambo ambalo limechangia kutinga hatua hiyo.
More Stories
Samia awazawadi Stars milioni 700/-
Samia atoa bilioni 8/- kukarabati viwanja vya CHAN, AFCON
Rasmi Chatsoko mdhamini mkuu wa Goba Hills Marathon 2025