December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Milioni 3.4 wahofiwa kukumbwa na njaa

YANGON, Zaidi ya watu milioni 3.4 nchini Myanmar wanaweza kuingia katika hatua za wasiwasi za ukosefu wa chakula kwa miezi sita ijayo na wanahitaji msaada.

Hayo yamesemwa na Marcus Prior ambaye ni Naibu Mkurugenzi wa WFP nchini humo kupitia mahojiano na UNnews.

Kupitia mahojiano hayo, Prior amesema, WFP imekuwa na wasiwasi sana kwa muda mrefu juu ya hali ya uhakika wa chakula nchini Myanmar na umaskini uliokuwepo hapo awali uliochangiwa na athari za virusi vya Corona (Covid-19) hasa katika maeneo ya mijini na mzozo wa kisiasa nchini humo.

Amesema, hali ni ngumu kwa watu wengi kwani watu wamekuwa wakihama katika eneo la Yangon. “Na viwanda vingi kwa sasa vimefungwa au vinafanya kazi kwa kiwango cha chini sana na mfumo wa benki umepooza nusu, na sio kawaida kuona watu wakipanga foleni katika foleni ndefu ili tu kuchukua pesa,”amesema.