Na Aveline Kitomary,TimesMajira oneline,Dar es Salaam.
LISHE bora kwa wanawake ni muhimu kwani husaidia kuwa na matokeo mazuri ya ujauzito na kufanikisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama.
Hali nzuri ya lishe inatakiwa kujengwa tangu mama akiwa mtoto kabla ya kupata ujauzito,wakati anapokuwa mjamzito na baada ya kujifungua
Mwanamke mbaye anajiandaa kupata ujauzito anahitaji mlo kamili unaotokana na makundi matano ya chakula kwani humpatia nguvu na virutubishi vyote vinavyohitajika kwaajili yake na mtoto aliyeko tumboni.
Lishe humuwezesha mwanamke kukua na kujengeka kimaumbile hivyo kumwezesha kuzaa kwa usalama na hatimaye kuweza kumnyonyesha na kumtunza mtoto vizuri.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), wanawake walio katika umri wa kuzaa ni wale wenye miaka 15 hadi 49 katika umri huu viungo vya uzazi vya mwanamke hupevuka kiasi cha kuweza kubeba ujauzito na kujifungua.
Takwimu za utafiti hali ya kidemografia,Afya na viashiria vya malaria za mwaka 2051-16 zinaonesha kuwa asilimia 7 ya watoto wanaozaliwa nchini Tanzania wanakuwa na uzito pungufu (chini ya kilogram 2.5).
Lishe bora kwa mawanamke aliye katika umri wa kuzaa husaidia kuimarisha kinga mwili dhidi ya magonjwa na upungufu wa damu ambao unaweza kusababisha kupoteza maisha wakati wa kujifungua.
Faida nyingine za kuwa na damu ya kutosha wakati wa ujauzito ni kuzuia tatizo la kuzaa mtoto mwenye uzito pungufu,kuzaa mtoto njiti na kuzaa mtoto mfu.
Pia husaidia kuzuia tatizo la kuzaa mtoto mwenye ulemavu wa viungo na ulemavu wa akili kutokana kutokana na ukosefu wa madini joto wakati wa ujauzito.
CHANGAMOTO ZA LISHE
Kwa Mujibu wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania(TFNC), Takwimu zilizopo zinaonesha kuwa wanawake walio katika umri wa kuzaa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa damu,magonjwa,utapiamlo,mila na desturi potofu na mimba za utotoni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Dkt.German Leyna anasema ugonjwa wa malaria unachangia tatizo la upungufu wa damu miongoni mwa wanawake walio katika umri wa uzazi .
“Ili kukabiliana na tatizo hilo serikali inatoa bure chandarua kwa wanawake wajawazito ili kujikinga takwimu zinaonesha kuwa ni asilimia 54 tu ya wajawazito wanatumia chandarua chenye dawa pamoja na hayo Serikali inatoa vidonge vya madini chuma na aside ya foliki kwa wanawake wajawazito ili kuhakikisha wanakuwa na damu ya kutosha.
“Changamoto zingine zinazowakabili wanawake walio katika umri wa uzazi ni utapia mlo wa ukondefu ,uzito uliozidi na kukithiri huku takwimu zikionesha kuwa ailimia 10 ya wanawake walio katika umri wa uzazi wana ukondefu ,asilimia 18 wana uzito uliozidi na asilimia 10 wanauzito uliokithiri,” anaeleza.
Dkt.Leyna anasema athari zake ni kuongezeka kwa uwezekano wa matatizo ya kiafya akati wa kujifungua kwani uzito uliozidi unaweza kusababisha mimba kuharibika pamoja na mtoto kuzaliwa akiwa mfu.
“Uzito unaongeza tatizo la shikizo la juu la damu na uwezekano wa kupata kisukari wakati wa ujauzito,wanawake wenye uziti pia wanauwezekanao mkubwa wa kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida ikilinganishwa na wenye uzito wa kawaida .
“Pia utapiamlo wakati wa ujauzito unaongeza uwezekano wa kuzaa watoto wenye matatizo ya mgongo wazi,vichwa vikubwa na midomo iliyopasuka kutokana na mtoto aliyeko tumboni kushindwa kupata kiasi cha kutosha cha vitamini ya acid ya foliki .
“Watoto wanaozaliwa na wanaweke wenye tatizo la kisukari wakati wa ujauzito wanakabiliwa na uwezekano mkubwa wa kuwa na uzito uliozidi na kisukari wakati wanapokuwa watu wazima,”anabainisha.
MILA NA DESTURI
Dkt.Leyna anasema changamoto nyingine ni mila na desturi za kijamii ambazo zinaathiri hali ya lishe .
“Miongoni mwa changamoto hizo ni nafasi ya mwanamke katika jamii ambapo anakabiliwa na kazi nyingi za uzalishaji mali na nyumbani kama malazi ya watoto na matunzo ya familia kwa ujumla.
“Hii inasababisha wanawake walio katika umri wa kuzaa kukabiliwa na umaskini wa muda hali inayosababishwa washindwekutekeleza kikamilifu tabia zinazoboresha lishe yao na hivyo kupata utapiamlo,”anaeleza Dk Leyna.
ATHARI ZA MIMBA ZA UTOTONI
Mmoja wapo ya matatizo yanayaowakabili wanawake walioko katika umri wa uzazi ni uwepo wa idadi kubwa ya wasichana balehe wanaopata mimba za utotoni.
Ingawa umri wa uzazi ni kuanzia miaka 15 had 49 ushahidi unaonesha kuwa msichana aliye katika balehe kati ya miaka 10 hadi 19 bado yupo katika kipindi cha ukuaji hata kama viungo vya uzazi vimepevuka.
Mtaalamu wa lishe Adeline Munuo anasema kitendo cha kubeba ujauzito katika umri mdogo(chini ya miaka 20) kinaweza kusababisha athari mbalimbali za kiafya wakati wa kujifumgua.
“Baadhi ya athari hizo ni kuota tatizo la fistula,uwezekano mkubwa wa kushindwa kujifungua,kuzaa mtoto mfu,kupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua na hata kupoteza maisha kutokana na matatizo wakati wa uchungu na kujifungua.
“Kingine ni kushindwa kutimiza majukumu ya kimalezi kwa watoto kikamilifu ,inasababisha wasichana kukosa elimu na kueleke kupata athari za kiuchumi na umasikini wanapokuwa watu wazima,”anabainisha Munuo.
HII NI LISHE INAYOFAA
Kwa mujibu wa Munuo anasema jamii inapaswa kuhimiza mabadiliko ya tabia,desturi na mitazamo inayoathiri afya ya wanawake walio katika umri wa kuzaa.
“Taratibu za ulaji zinatakiwa kuzingatiwa na ulaji unaofaa kabla ya ujauzito ni mlo kamili wenye mchanganyiko wa vyakula kutoka katika makundi matano ya vyakula ili kuupa mwili virutubishoi vyote vinavyo hitajika kwa afya.
“Tabia ya ulaji unaofaa kama vile vyakula vya asili ya nafaka ,mizizi na ndizi,vyakula vya asili ya wanyama na mikunde, mbogamboga, matunda, mafuta, sukari na asali kwa kiasi kidogo ni muhimu sana ,kunywa maji safi angalau glasi nane au lita 2 kwa siku na matumizi ya chumvi yenye madini joto.
Anasema wakati wa ujauzito wanawake wanapaswa kuendeleza tabia ya ulaji unaofaa ili kutosheleza mahitaji na virutubishi kukidhi mahitaji ya mtoto anayekua na kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya maradhi.
“Mjamzito anatakiwa kula milo mitatu yenye chakula cha kutosha katika makundi ya vyakula ,kula vitafunywa au asusa kati yam lo na mlo walau mara moja kwa siku,anatakiwa ale matunda na mbogamboga katika milo,maji safi .
“Mjamzito aepuke kunywa chai,kahawa ,soda za aina ya cola pamoja na mlo kwani huzuia kufyonza ya chuma na kuweza kusababisha upungufu wa damu ,kula vyakula vilivyoongezewa virutubishi ikiwemo mafuta ya kula ,unga wa ngano na wa mahindi ulioongezewa vitamin na madini na tumia unga na nafaka zisizokobolewa.
“Meza vidonge vya kuongeza damu kama ilivyoshauriwa na mtaalamu wa afya,”anaeleza.
Munuo anasema ulaji unafaa unatakiwa kuendelea hata baada ya kujifungua ili kufanikisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama .
“Sanjari na lishe wanawake walio katika umri wa uzazi wanapaswa kutumia wahudumu wa afya ya uzazi na mtoto kwa wakati ili waweze kupata huduma zinazoboresha lishe na afya yao kwaajili ya uzazi salama.
“Ni muhumu kutumia huduma hizo mapema mara baada ya kugundua ni mjamzito kwani wakichelewa hawawezi kupata huduma kamilifu.
“Anatakiwa kuhudhuria kliniki mara tu anahisi ni mjamzito na kuhudhuria katika kipindi chote cha ujauzito ili kupata huduma zote ikiwemo ushauri nasaha na elimu,kutumia vidonge vya madini chuma na aside ya foliki katika kipindi chote cha ujauzito,dawa za minyoo,kutumia kinga tiba za malaria ikiwa ni pamoja na kulala kwenye chandarua,”anasema.
mwisho
More Stories
Ubunifu wa Rais Samia kupitia Royal Tour unavyozindi kunufaisha Tanzania
Rais Samia anavyojenga taasisi imara za haki jinai kukabilina na rushwa nchini
Rais Dk. Samia alivyowezesha Tanzania kuwa kinara usambazaji umeme Afrika