January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Miili ya wafanyakazi watano TRA yaagwa, vilio vyatawala

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira,Online, Mbeya

MIILI ya wafanyakazi watano wa Mamlaka ya Mapato (TRA) waliofariki kwa ajali ya gari jana imeagwa, huku simanzi ikiwa imetawala miongoni mwa waombolezaji, wakiwemo ndugu, jamaa na marafiki.

Wafanyakazi hao walifariki baada ya gari walilokuwemo wakilitumia kufukuza gari lililosadikiwa kuwa na magendo kugonga kwa nyuma Fuso.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Janeth Magomi, ajali hiyo ilitokea katika barabara ya Tunduma- Mbeya katika kijiji cha Hanseketwa saa 11:45 alfajiri.

Wafanyakazi wanne walikuwa wa Mkoa wa Mbeya na mmoja wa Tunduma mkoani Songwe na walikuwa katika doria na walihisi gari moja kupakia mzigo wa magendo na kuamua kulifukuza.