November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Miaka 61 ya Uhuru,watu takriban milioni 250 wanazungumza Kiswahili ‘Kiswahili kipo juu

Na Joyce Kasiki,Timesmajia online

‘Kiswahili kipo juu’ni maneno ya Menna Yasser raia kutoka nchini Misri ambaye ana shahada ya kwanza ya lugha ya Kiswahili na kwamba lugha yake ya kwanza ni Kiswahili na lugha ya pili ni kijerumani

Kwa upande wa kazi Menna anasema yeye ni  mtangzaji wa radio kwa lugha za Kiswahili na kiarabu lakini pia mimi ni mwalimu Kiswahili nchini Misri na pia anafundisha watu wengi Afrika na nje ya Bara la Afrika.

Anasema,ni mwandishi wa kitabu cha kwanza kilichoandikwa na Mmisri kwa lugha ya Kiswahili .

Akizungumza mbele ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe Menna anasema katika kuelekea maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania ,wananchi na nchi kwa ujumla haina budi kujivunia lugha ya kiswahili na kuona namna ya kuiboresha lugha hiyo ambayo anasema sasa inapaa ndani nje ya nchi ya Tanzania.

Mennar Yasser Mmisri anayejivunia lugha ya Kiswahili

“Tupo hapa ili kusherehekea siku ya kumbukumbu ya miaka 61 ya uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuona jinsi ya kuboresha lugha ya Kiswahili kama utambulisho wetu ,

“Utambulisho wa mtu ni lugha yake ,utambulisho si kujulikana unatoka wapi bali utatambulika kwa lugha yako,lakini kuna kitu kinaitwa ukoloni maomboleo unaokuwa ndani ya mawazo,yaani usifikiri kama ukizungumza kingereza utaonekana ni mtu mstaarabu sana  ,au usifikiri kama wewe ukiacha mavazi yako na kuvaa kama Mzungu utakuwa mstaarabu hapana,unapaswa kuhifadhi utambulisho wako wewe mwenyewe “anasema Menna

Aidha anasema zipo  nchi nyingi za ndani na nje ya bara la Afrika wanajua Kiswahili na wapo wanaopenda kujifunza Kiswahili kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuona ni sehemu ya burudani huku akijitolea mfano yeye mwenye kwamba anapenda kuwa na lugha nyingi na kwamba nafahamu na kuzungumza lugha zaidi ya tatu.

Kwa mujibu wa Menna ,weninge wanapenda kujifunza lugha mbalimbali kwa ajili ya uwekezaji huku akisema nchini  Tanzania kuna wamisri wengi  wanafanya uwekezaji wao huku akisema wanaweza kufanya vipi uwekezaji bila ya kufahamu lugha ya Kiswahili.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe akizungumza wakati ya hafla ya kukabidhi bango la Kiswahili kwenda kupandishwa Mlima Kilimajaro kama sehemu ya maadhimisho kuelekea sherehe ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania

“Kama nilivyo mimi , nafundihsa Kiswahili na watu wengi sana wanapenda kujifunza Kiswahili ambacho sasa kipo juu sana,mfano Nchi ya sudani Kusini sasa kiarabu ni lugha ya kwanza,kingereza lugha ya pili na lugha ya tatu ni Kiswahili.”anasema na kuongeza kuwa

“Sisi tunahitaji kujivunia sana lugha hii na kuiboresha ,acha kingereza acha kifaransa,acha lugha zetu ,tujivunie Kiswahili.”

Anasema,katika nchi ya Misri mahali pengi wanafundisha lugha ya Kiswahili na kwamba vyuo vikuu karibu vinne vinafundisha lugha hiyo ya Kiswahili na kwamba kati ya vyuo hivyo kimoja kimeanza kufundisha Kiswahili tangu mwaka 1964.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe anasema Wizara imeona  kuna kila sababu ya kutambua Kiswahili kwenye maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru huku akisema wameamua kupandisha bango la Kiswahili Mlima Kilimanjaro ambapo kaulimbiu ya maadhimisho kwa upande wa Kiswahili ni ‘kiswahili Kileleni ‘.

Anasema kitendo cha kupandisha bango la Kiswahili Mlima Kilimanjaro pamoja na kauli mbiu hiyo vinalenga  kupanua wigo wa  upendo uliosemwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wakati wa kuwasha Mwenge na kuupandisha Mlima Kilimanjaro huku akisema upendo huo usambae kwenye suala la Kiswahili .

“Kwa hiyo wakati tukielekea kwenye maadhimisho ya kusherehekea miaka 61 ya Uhuru ambapo siku hii husherehekewa Desemba 9,ya kila mwaka ,Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ambao pamoja na mambo mengine pia tuna dhamana ya kufundisha lugha ya Kiswahili,tutapandisha bango la Kiswahili kwenye Mlima Kilimanjaro tukiwa na lengo la kueneza Kiswahili kwa Mataifa mengi zaidi kuliko sasa .”anasema Profesa Mdoe

Kwa mujibu wa Profesa Mdoe ,hadi hivi sasa Kiswahili kina wazungumzaji takribani milioni 250 huku akisema pamoja na watanzania karibu wote kuzungumza kiswahili lakini pia yapo Mataifa likiwemo Taifa la Kenya Uganda,Mashariki mwa Kongo,Sudani Kusini,Malawi,Zambia na Mataifa mengine ambayo hatupo jirani nayo kama Misri,yanazungumza Kiswahili.

“Nimefurahi kusikia kwamba Kiswahili kinapendwa na watu wengi ,tumepata ushahidi kutoka kwa mwenzetu wa Misri ,kwa hiyo sisi kama wizara ya elimu tunao wajibu kuendelea kukikuza Kiswahili kwa njia ya kutoa mafunzo kwa watu wengi kadri iwezekanavyo,

“Pia nafurahi kuona kwamba kuna vyuo visivyopungua  150 vinavyotoa mafunzo ya kiswahili maeneo mbalimbali,lakini kuna redio na televisheni zisizopungua 300 ulimwenguni ukiacha za Tanzania ambazo zinarusha vipindi kwa lugha ya Kiswahili ,kwa maana hiyo Kiswahili kimepanuka “anasema Profesa Mdoe

Anasema,kwa muktadha huo wa kuendeleza na kutoa mafunzo kwa watu wengi kadri iwezekanvyo vyuo vya Tanzania vina makubaliano na vyuo vingine vya nje kwa ajili ya kuendelea kufundisha Kiswahili na kwamba hata wizara ina mikataba kama minnne hivi na wizara za zinazohusu mafunzo kuhusiana na masuala ya Kiswahili.

Profesa Mdoe anatoa wito wakuu wa taasisi na wakuu wa Idara waongeze kasi katika maongezi  yanayoendelea ili wakamilishe  kwa haraka na hatimaye mafunzo ya lugha ya Kiswahili ianze kufundishwa katika nchi wanazoingia mikataba.

Kila ifikapo Desemba 9,ya kila mwaka ,watanzania hushehekea siku muhimu ya kupatikana kwa uhuru wao uliopatikana mwaka 1961 ambapo sasa ni miaka 61 tangu kupatikana kwa Uhuru huo.