January 18, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Miaka 61 ya Uhuru

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene  amesema nchi imepiga hatua kubwa katika ujenzi wa maendeleo ambayo ni shirikishi na yamelenga watu.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu katika kilele cha maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanzania Bara kilichofanyika Kibakwe Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.

“Katika ujenzi wa maendeleo ukisema ujenzi wa sekondari za kata, ujenzi wa vituo vya afya ujenzi wa barabara vyote vimetekelezwa kwa kushirikisha wananchi.”

Kauli mbiu ya miaka 61 ya uhuru ambayo inasema, Amani na Umoja ni nguvu ya maendeleo yetu.” Imetusaidia kutimiza shabaha zetu.

“Mabadiliko ya kisiasa, mabadiliko ya kiuchumi, Mhe. Rais amepeleka maendeleo hayo kwa watu na maendeleo ya watu yanahitaji rasilimali fedha,” alisema waziri .

Sisi watanzania tuna misingi yetu kila awamu inayoingia  inategemea misingi ya awamu iliyopita ndio maana tumefika hapa tulipofika.

 “Watanzania wanapenda furaha watanzania hawapendi hofu watanzania ni watii kwa mamlaka, tuendelee kuheshimiana na kuipenda nchi yetu.”

Hata wenye mawazo mbadala Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua mipaka ndio maana anazungumzia R-nne watu wawe na utaratibu wa maridhiano; maelewano, kujenga upya, na kuendelea mbele.

“Tunaiona Tanzania iliyobadilika sana kimaendeleo, lakini imebakia na misingi ile ile iliyoachwa na waasisi wa Taifa letu katika mioyo ya watu.”

Tulivyopata uhuru falsafa ya Baba wa Taifa alisema, Uhuru ni kazi ndio maana wananchi wamejikita katika kufanya kazi.

Awali Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Mhe. George Fuime amesema nchi imepiga hatua kwenye miundo mbinu ya Mawasiliano.

“Ujenzi wa miundo mbinu ya afya, ujenzi wa miundo mbinu ya elimu, mabadiliko haya yameasisiwa na viongozi wetu kutokana  na Amani na utulivu uliojengwa na wazee wetu.”

Naye muwasilishaji mada Mwl Charles Malugu amesema serikali ya awamu ya sita imefanya ujenzi wa sekondari vyumba 20000, na ujenzi wa vyumba 3000 kwa shule shikizi  ambao utasaidia wanafunzi wa kidato cha kwanza na wanafunzi wa darasa la kwanza kuanza masomo bila kuwa na kikwazo cha aina yoyote.

“Serikali ya awamu ya sita imeruhusu wanafunzi walikatisha masomo kutokana na ujauzito, kuendelea na masomo ili wasikatize ndoto zao.”

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene
Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akishiriki kupanda miti katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akikabidhi vyeti kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika uandikaji wa insha kuhusu miaka 61 ya Uhuru.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpwapwa Bi. Mwanahamisi Ally akishiriki kupanda miti katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanzania Bara.