Esther Macha, TimesmMjira Online, Mbeya
NAIBU waziri wa maji Mhandisi, MaryPrisca Mahundi amesema kuwa wanahitaji mageuzi makubwa kwenye wizara hiyo ili yale yaliyokuwa yakizungumzwa huko nyuma ifikapo 2025 wizara iwe na sura tofauti kabisa.
Mhandisi Mahundi amesema hayo wakati akizungumza na wafanyajazi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Jijini Mbeya kuhusu malalamiko mengi ya kero za maji katika maeneo mbalimbalib ambayo yanaweza hata kuwanyima kura.
“Mimi ni mwanasiasa nimepita maeneo mbali nchini kumuombea kura rais na kulikuwa na malalamiko mengi na vitisho, tunahitaji kufanya mabadiliko na mageuzi ya kiutendaji kwa makusudi kabisa na wale wenzetu wa ufundi fanyeni kazi kwa uaminifu,” amesema Mhandisi Mahundi.
Amesema kuwa, watu wa ufundi wafanye kazi kwa moyo kwa kudhamilia mabadiliko huduma ya maji inatakiwa kuwa karibu na makazi ya wananchi na kusema kwamba wasikubali kufelisha miradi ya maji kwa makusudi.
“Tusimwangushe rais wetu mama Samia Suluhu Hassan kwa sababu anaitendea haki sana Wizara Maji yetu na bajeti kamili tumewakilisha bungeni ikapitishwa na akaona haitoshi akaongeza bilioni 207 kwa akili ya kawaida anataka tuingie kazini anataka kuona mabadiliko,tusiishe tupewa fedha harafu hatufanyi kazi kwa bidii,tusimamie miradi na ikamilike kwa wakati,” alisema Naibu Waziri.
Akizungumzia kuhusu mahusiano kwa wateja, Mhandisi Mahundi amesema kuwa amekuwa akipokea jumbe nyingi kutoka kwa wateja wakilalamikiwa wafanyakazi kutokawa na lugha rafiki hivyo wanapaswa kubadilika.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji na usafi wa mazingira, Edina Mwaigomole amewataka watumishi wa mamlaka hiyo kuchapa kazi kwa kuiga mfano wa Naibu Waziri.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa mamlaka yhiyo, CPA Gilbert Kayange amesema kuwa Katibu Mkuu Wizara hiyo amekubari kuongeza fedha za mradi wa maji hivyo watahakikisha wanatatua changamoto ya maji inayokumba baadhi ya maeneo.
More Stories
Ushiriki wa Samia G20 wainufaisha Tanzania
Dkt.Tulia ashiriki ibada, asisitiza waumini kushiriki uchaguzi serikali za mitaa
Polisi yaonya vyama vya siasa