November 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mhandisi Mahundi: Wazazi kuweni na maadili mema kwa watoto

Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya

NAIBU  Waziri wa Maji Mhandisi, Maryprisca Mahundi( Mb)amewata wazazi kuwalea watoto wa katika maadili ili waweze kufikia ndoto zao badala ya kuwaachia walezi pekee ambao huwafanyia ukatili ikiwemo ubakaji na ulawiti.

Mahundi amesema hayo leo wakati  wa  hafla ya Frola Mnyandavila dereva wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya.

“Wazazi wengi wamekuwa wakikwepa majukumu ya malezi kwa kuwaachia walezi ambao baadhi huwafanyia ukatili pindi wawapo kazini vikiwemo vya ulawiti na ubaki”amesema Mahundi.

Aidha amesema Frola ametoa somo kwa jamii kwa kutokata tamaa pindi wanapokutana na changamoto bali wazitumie changamoto kama fursa.

Kupitia changamoto alizopitia  dereva huo  ameamua kumsomesha mtoto mwenye ulemavu anayesoma shule ya Hayanga kwa mahitaji yote sambamba na kumpatia baiskeli mwendo kama sehemu yake ya shukurani.

Frola amepitia mafunzo mbalimbali yakiwemo ya udereva ambayo yamemwezesha kujikimu kimaisha na kumudu kuwasomesha watoto.

Kwa upande wake ,Dereva Frola Mnyandavira amesema kwamba njia pekee ya mzazi ni kuhakikisha watoto wanakuwa katika malezi mazuri na kuwaacha na walezi pekee.