Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbarali
WANAWAKE katka halmashauri ya wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya
wametakiwa kuungana kwa pamoja katika kutumia ubunifu wao pamoja na
Teknolojia kwa mambo mazuri ya kimaendeleo pamoja na kukemea vitendo
vya ubaguzi na udhalilishaji na uhalifu dhidi ya mwanamke kwani nchi
inahitaji wanawake wabobezi na weledi katika fani mbali mbali .
Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu waziri wa maji Mhandisi Maryprisca
Mahundi (Mb) wakati alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya
sikukuu ya wanawake duniani ambayo kiwilaya imefanyika katika viwanja
vya shule ya msingi Ibala iliyopo Mjini Rujewa .
‘’Hapa nipende kurejea picha mbali mbali zilizochorwa na mwanafunzi
zikionyesha uwezo wa mwanamke ,amefanya kitendo kizuri cha
kudhihilisha umma kuwa watoto wa kike wana utambuzi kwa hiyo ninaomba
watoto wa kike mlio[pata fursa ya kupata nafasi za kimasomo nendeni
mkasome pendeni shule licha ya kuwa na vikwazo’’amesema Mhandisi
Mahundi .
Hata hivyo Naibu waziri huyo amesema kuwa licha ya elimu bure kutolewa
na serikkali lakini bado kuna wazazi bado ni kikwazo na serikali
itaendellea kushughulika na wazazi ambao wanakwamisha juhudi za mtoto
wa kike katika harakati za kujipatia elimu.
Hata hivyo Mhandisi Mahundi amesema kuwa serikali itahakikisha
inafanya juhudi kuhakikisha inapata mwanafunzi anayejitambua kama
aliyechoora picha mbali mbali na kazi mbali mbali zikionyesha uwezo
wa mwanamke katika jamii wanawake Mungu amewabariki kufanya shughuli
moja kwa dakika moja .
‘’Lakini tuna Mwanamke ambaye ni kielelezo kwa dunia Tanzania
ambaye ni Mh.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan lakini tunashukuru Mungu
tuna mihimiwili mitatu ya serikali mihimili miwili inamilikiwa na
wanawake mashuhuri , wanawake mahili wanaowatoa kimasomaso wanawake
wenzao,mhimili mkuu wa serikali kuu Dkt. Samia , mhimili wa Bunge ni
Dkt. Tulia Ackson .
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya
Mbarali ,Missana Kwangura amesema kuwa halmashauri itaendelea
kuhakikisha wanawake wanapata mikopo sababu ni maelekezo ya serikali
na Bunge .
Missana amesema kuwa kwa mwaka fedha 2021 wamekopesha vikundi vya
akina mama 68 ambavyo vilikuwa na wanachama 577 na wamekopesha mil.409
kwa mwaka uliofuata wamekopesha vikundi 57 jumla ya wanachama 682
walikopeshwa zaidi ya mil.623,2022/2023 wamekopesha vikundi 24 jumla
ya wanachama 219 ambao walikopeshwa zaidi ya mil 282.
Zabibu Baharam ni Mwenyekiti Jumuiya ya umoja wa wanawake wilaya ya
Mbarali (UWT) amesema kuwa wanawake wa wilaya ya Mbarali hakuna
mwanamke anayezunguka bila ya wizara maalum kila mwanamke anajitambua
hivyo tunaomba Naibu waziiri wa maji uendelee kutuombee mikopo baadhi
hawana mitaji wala mashine ili waweze kupata mikopo.
‘’Mimi kama Mwenyejkiti wa wanawake wilaya ya mbarali ninaendelea
kuwasimamia kupata mikopo na kazi inafanyika kwa baadhi wanaendelea
na biashara , lakini wakati tukiwa tunaendelea na biaashara zetu basi
ndugu zangu wanawake wenzangu tuwalee watoto wetu katika maadili
yaliyo mema watoto wetu wanafanyiwa vitu visivyo vizuri linda mtoto
toka anatokea nyumbani ‘’amesema Mwenyekiti huyo .
Jeremiah Makao ni Kaimu Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mbarali
na Diwani wa Kata ya Rujewa amevitaka vikundi vya wanawake vyote
vilivyopo wilayani humo ambavyo vinajishughulishja na ujasiliamali
kuhakikisha kuwa kukidhi vigezo ili viweze kupatiwa mikopo.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini