December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mhandisi Mahundi kuwainua kiuchumi Mama Ntilie 700 Mbeya

Na Esther Macha,Timesmajira Online, Mbeya

NAIBU Waziri wa Maji ,Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema kuwa atawafikia Mama Ntilie 700 wenye mitaji midogo kuanzia 15,000 mpaka 20,000 ili kuwainua kiuchumi .

Mhandisi Mahundi amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari wanawake waliotaka kujua lengo la Tamasha la Mama Ntilie (Mama Ntilie Festival),ambalo linatarajiwa kufanyika kesho(Octoba 4,2023) ili kuendelea kuwainua wanawake ambao wana uchumi wa chini.

“Mama Ntilie Festival linakuja msimu maalum kwa ajili ya mama ntile na walengwa wakuu ni wale ambao wanatamani kuwa wakubwa lakini wameanza mdogo mdogo ambao wana mitaji kuanzia 15,000 mpaka 20,000,wanapika vyakula vyao na kuuza stendi za mabasi,maeneo ya kutengenezea magari (Gereji ) pamoja na maeneo panapofanyika ujenzi unaoendelea,“ amesema Mhandisi Mahundi.

“Nataka kuona mwanamke ambaye ana mtaji mdogo na ameupata kupitia vikoba vya mtaani ambako wanapeleka kuanzia 200 mpaka 500 sababu uwezo wake ni mdogo anaishia kukopa ili apate mtaji wa 15,000,wanainuka kiuchumi kwa Mimi kuwezesha mitaji yao kukua,”ameeleza.

Mhandisi Mahundi amesema kuwa October 4 ,mwaka huu wanaenda kufungua rasmi tamasha la Mama Ntile ambapo kwa Rungwe watawafikia wanawake 100 huku lengo ni kufikia wanawake, 700 wa majimbo yote saba ya Mkoa wa Mbeya .

Ambapo sanjari na hayo watapata elimu ya mapishi kutoka Chuo cha Ufundi Stadi (VETA ) ya namna nzuri ya kupika chakula kizuri chenye radha tofauti na virutubisho vyote.

Aidha ameeleza kuwa washindi watano ambao watapatikana katika tamasha hilo watapatiwa fedha kwa ajili ya kuongeza kwenye mtaji huku wanawake wote 100 waliopika chakula kila mmoja atapatiwa jiko la grsi lenye kilo sita ambalo atatumia kwenye shughuli zake za mama ntilie lengo likiwa ni kuona kuwa Rais Samia anaungwa mkono matumizi ya nishati safi ambayo inatunza mazingira kwa kuokoa ukataji wa miti kwa wingi kwa ajili mkaa na kuni .

Amesema kuwa Tanzania inaingia kwenye historia ya wanawake kwenye familia na biashara za chakula wakiacha ukataji wa miti kwa ajili kuni na mkaa badala yake wanatumia nishati safi hali itakayosaidia taifa kujabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Diwani wa viti maalum Kata ya Makongolosi Sophia Mwanauta amesema kuwa tamasha hilo linaenda kuleta hisia kwa wanawake wa hali ya chini kiuchumi ambao wamekuwa wakijishughulisha na kazi za Mama Ntilie kwa kutegemea vikoba vya kuchangishana mtaani .