Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya
Naibu Waziri wa Maji,Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema kuwa Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU),Dkt.Tulia Ackson amewahishima wanawake huku akwataka wanawake mkoani humo kuendelea kushikama.
Mhandisi Mahundi ameyasema hayo wakati akitoa salamu kwa wanaMbeya baada ya mapokezi ya Rais wa IPU,Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt.Tulia Ackson.
“Tunafuraha Dkt.Tulia ametuheshimisha wana Mbeya wanawake tunaweza,tunasimama naye, tunasema asante Rais Samia Suluhu Hassan umetupa heshima kubwa wana Mbeya,naomba wanawake wote tuendelee kuwa pamoja, “amesema Mhandisi Mahundi .
Mbunge wa Jimbo la Mbarali Bahati Ndingo,amehaidi kumlinda kwa nguvu zote Rais IPU, Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini Dkt.Tulia Ackson.
“Tuna kila sababu wana mbeya kujivunia ushindi huu,hatuna neno nzuri la kumshukuru Rais Dkt Samia tunasema asante hii ni lulu kwetu tutaitunza maana ameheshimisha wanawake,”amesema Ndingo.
Mbunge wa Jimbo la Makete Festo Sanga,amesema kuwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 umekwisha Mbeya hawana sababu ya kimdharirisha Rais wa IPU kwa kumsimamisha na mgombea mwingine.
“Itawekwa fomu moja tu kazi inakuwa imeisha hatuna ushindani tena katika uchaguzi mkuu ujao,” amesema Mbunge huyo.
More Stories
Kamati ya Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini yagawa vifaa vya ujenzi
Hatma mrithi wa Kinana kupatikana
Mrithi wa Kinana CCM kujulikana katika Mkutano Mkuu wa Jan 18/19