December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mhandisi Mahundi aridhishwa utekelezaji mradi wa ujenzi bwawa la Kidunda

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online,Pwani

Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ametembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa kimkakati wa ujenzi wa bwawa la Kidunda unaogharimu kiasi cha bilioni 329.47 huku akirudhishwa na kasi ya utekelezaji wake.

Mahundi amesema kuwa mradi huo wa kimkakati wenye lengo la kuhakikisha maji yanapatikana kipindi chote cha mwaka kutoka mto Ruvu ambao ni chanzo kikuu cha maji jijini Dar es Salaam na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani.

Ameeleza kuwa mradi huo ukikamilika utasaidia kukabiliana na changamoto ya ukame ambao umekuwa ukijitokeza mara kwa mara na kusababisha upungufu mkubwa wa maji.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA ,Kiula Kingu ameeleza kuwa mradi huo unajumuisha ujenzi wa bwawa la kuhifadhi maji lenye mita za ujanzo milioni 190,ujenzi wa kituo cha kufua umeme wa megawati 20,ujenzi wa njia ya msongo mkubwa wa umeme kutoka Kidunda hadi Chalinze umbali wa kilomita 101 pamoja na ujenzi wa barabara ya kiwango cha changarawe yenye urefu wa kilomita 75 kutoka Ngerengere hadi kidunda.

Amesema kuwa hadi sasa Mkandarasi wa ujenzi na Mtaalam Mshauri atakayesimamia ujenzi ameshapatikana na kiasi cha bilioni 49.4 ambazo ni fedha za ndani zimetolewa ikiwa ni malipo ya awali ili kuanza ujenzi wa bwawa hilo.