May 20, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mhandisi Mahundi apongeza  umoja wa wanawake Iringa  kuthamini kazi zinazofanywa na viongozi

 
Na Esther Macha, Timesmajira Online, Iringa 

KATIKA kuthamini kazi kubwa anazofanya  Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ,Rais Samia  Suluhu Hassan umoja wa wanawake mkoa wa Iringa umefanya  kongamano la wa kumpongeza Rais  Samia kutokana na juhudi kubwa anazofanya  katika kuwaletea maendeleo watanzania .

Imeleezwa kuwa Rais Samia  amekuwa akiwatia moyo wanawake wote kutokata tamaa  katika suala zima la kujiletea maendeleo.

Hata hivyo Kongamano hilo liloandaliwa  na umoja wa wanawake mkoa wa Iringa (UWT)pia walitumia fursa hiyo kumpongeza Spika wa bunge  Dkt.Tulia Akson  Kwa kuchaguliwa kuwa spika wa bunge la jamhuri  ya muungano wa Tanzania.

Mgeni rasmi kwenye kongamano hilo, Dkt.Tulia Akson aliwakilishwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya ,ambaye pia ni Naibu Waziri wa afya maji Mhandisi,Maryprisca Mahundi ambaye aliwashukuru wanawake wa UWT mkoa wa Iringa  kwa kuthamini na kuenzi kazi zinazofanywa na viongozi katika  kuwaletea maendeleo wananchi.

Hata hivyo Mhandisi Mahundi aliwasihi kuendelea kushirikiana na serikali ili wao kama wenye ilani utekelezaji wake uwe mzuri.

Aidha ameshukuru na kuwapongeza viongozi wa chama na serikali kwa jinsi wanavyoshirikiana kutekeleza ilani ya CCM ambayo walishirikiana kuinadi mbele ya watanzania.