Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel,amewaomba wananchi wa Mkoa huo kuwa na subira kwani changamoto ya upatikanaji wa maji ya uhakika inatarajiwa kupunguzwa na hatimaye kuwa historia.
Mhandisi Gabriel, amesema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi wa ujenzi wa chanzo kipya cha maji Butimba kilichopo wilayani Nyamagana mkoani Mwanza ambao unagharimu kiasi cha bilioni 69.
Amesema wananchi wamekuwa wakilalamika mara kwa mara kuwa maji hayatoshi,visima vidogo havitoshelezi mahitaji lakini katika hitaji kama hilo wana chanzo cha asili kikubwa Ziwa Victoria kama wanamwanza anaiona Mwanza yenye maji ya kutosha ipo njiani.
Ambapo amesema ,mradi huo ukienda vizuri na ratiba mwakani Februari ukakamilika,itasaidia kupunguza changamoto ya maji kwani mahitaji kwa sasa ni lita milioni 160 kwa siku huku chanzo cha maji cha Capripoint kilichopo sasa kina uwezo wa kuzalisha lita milioni 90 wakijumlisha na hicho cha Butimba ambacho mtambo wake wa kwanza ambao ujenzi unaendelea kitakuwa na uwezo wa kuzalisha lita milioni 40 watakuwa na lita za maji milioni 130.
“Tunabakia na uhitaji wa lita milioni 30 ili tujikute Mwanza tunakuwa na maji ya uhakika ni hatua nzuri za kimapunduzi hapa tulipo fikia kwaio kipande kidogo kitakacho bakia cha mahitaji na jitihada zinazofanya na serikali na wataalamu zinaenda vizuri hivyo wananchi wawe na subira wanasema yajayo yanafurahisha,”amesema Mhandisi Gabriel na kuongeza kuwa
“Niwatoe hofu wanamwanza waone nimekuja kama Mkuu wa Mkoa na baadhi ya wataalamu kujiridhisha kazi ambazo zinafanywa na Serikali ya awamu ya sita lakini ikizingatiwa chini ya Wizara husika ya maji,tumeona na tumeshuhudia hapa Mkandarasi nimemkuta yupo site lakini pia na wataalamu wake na kazi inaendelea,”.
Sanjari na hayo amesema, chanzo hicho kitakuwa na mitambo minne ya kusafisha maji, mtambo wa kwanza tayari ujenzi unaendelea vizuri na utakapo kamilika maji safi yatakayo patikana wanaweza sasa kuyapampu kuelekeza katika matenki ambayo yatakuwa yamejengwa kwa ajili ya usambazaji katika miji ambapo yatagusa zaidi Wilaya ikiwemo Wilaya mwenyeji ya Nyamagana katika maeneo ya Buhongwa na Igoma ambapo kulikuwa na changamoto za maji muda mrefu
,Misungwi yanaweza kufika kabisa upande wa daraja l la J.P.M mengine pamoja na Kisesa hivyo na watu wa Magu watanufaika na mradi huo mkubwa.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA) Mhandisi Leonard Msenyele, amesema mradi huo unagharimu kiasi cha bilioni 69 na unatarajiwa kukamilika Februari 2023 ambapo lengo lao kufikia muda huo Mkandarasi awe amewakabidhi mradi.
“Ni kweli Kuna changamoto ya maji katika Jiji la Mwanza, sehemu kubwa tunatoa maji kwa mgao lakini chanzo chetu cha Capripoint akitoshelezi mahitaji,kwani mahitaji ni milioni 160 uzalishaji ni lita milioni 90 hivyo kuwa na upungufu wa lita za maji milioni 70 hivyo lazima kufanyike mgao,”amesema Mhandisi Msenyele.
Amesema,chanzo hicho cha maji Butimba kina laini( mitambo) minne ya kuzalisha maji ambapo kila mtambo unauwezo wa kuzalisha lita za maji millioni 40 hivyo kufanya jumla kuwa na uwezo wa kuzalisha lita za maji milioni 160 na kutokana na ufinyo wa fedha wameanza na mtambo mmoja ambao ujenzi wake unaendelea.
“Fedha iliopo ni kwa ajili ya laini ya kwanza ya lita milioni 40 nyingine ni kwa mpango wa baadae,tukipata fedha jumla tutamalizia lita zote milioni 160,kazi imesha anza tulimkabidhi Mkandarasi mradi mwaka 2021 kwa maana atatekeleza kwa miezi 24, na katika mradi huu anafanya kazi ya kusanifu na kujenga ambapo kwa upande wa kusanifu ameisha kamilisha asilimia 90 na kujenga ujenzi yupo asilimia 12 tunaweka nguvu zaidi kumsukuma ili aweze kumaliza kwa wakati,”amesema Mhandisi Msenyele.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi