January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mgonja awataka Wanawake TAOWE wajikwamue kiuchumi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

AFISA Tawala wa wilaya ya Ilala Flora Mgonja amewataka wanawake wa TAOWE wajikwamue Kiuchumi katika kutafuta fursa mbali mbali ambazo zitawawezesha kupata masoko makubwa yatakayowawezesha kukuza mitaji yao.

Akizungumza wakati wa kuzindua shirika lisilo la kiserikali la TAOWE Afisa Tawala Flora Mgonja, aliwataka TAOWE washirikiane pamoja na kupendana katika kutekeleza majukumu yao ya shirika hilo ambapo Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ilala itawasaidia kwa kila hatua ili waweze kusonga mbele.

“Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ilala itawasaidia kwa kila hatua ili muweze kujikwamua shirika lenu nawaomba mpendane kwa pamoja na kufuata taratibu “alisema Flora.

Frola aliwapongeza Shirika la TAOWE kwa kusajiliwa na kutambulika kisheria na kufuata taratibu za nchi ambapo aliagiza Halmashauri ya jiji iwawezeshe shirika la TAOWE mkopo ili waweze kusonga mbele .

Alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ni mwanamke mwezetu hivyo tumuunge mkono wanawake wote katika utekelezaji wa Ilani na kuleta fursa mbali za kiuchumi na Maendeleo ya nchi yetu kwa sasa yamekuwa

Aidha wakati huohuo wanawake wa shirika la TAOWE kupinga vitendo vya ukatili ambavyo wanafanyiwa Jamii mbali mbali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa shirika la TAOWE Aminael Mshana, alisema shirika hilo limesajiliwa kwa mujibu wa sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali kupitia wizara ya maendeleo ya jamii jinsia Wazee ,na watoto na makundi maluum.

Mwenyekiti Mshana alisema shirika hilo lilianza na wanachama 40 kwa sasa wanachama 45 lengo la kuanzishwa kwa taasisi hiyo kukemea vitendo vya ukatili kwa mama na mtoto katika halmashauri ya wilayani Ilala.

Aidha alisema dhumuni lingine kuanzishwa kwa taasisi hiyo kuwaleta wanawake Wajasiriamali ili kukuza uelewa wao katika elimu,fursa na masoko ya kibiashara kwa kuwajengea uwezo wanawake ndani ya jamii kuhusiana na ujasiriamali, ujuzi ili wapate kujiajili na kusimama maslahi ya wanawake ili kujenga jamii yenye fursa zaidi kwa wanawake