November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mjumbe wa Halmashauri Kuuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iringa Mjini, Joseph Mgongolwa. (Na Mpiga Picha Wetu).

Mgongolwa amtaka Diwani kufuta kauli ya viboko wasioshiriki misiba

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iringa Mjini mkoani Iringa, Joseph Mgongolwa amemtaka Diwani wa Kata ya Mwangata, Edward Nguvu kufuta kauli ya kuwataka wasiohudhuria misibani wacharazwe viboko ili iwe fundisho kwa wengine.

Amesema, kauli hiyo imezua taharuki mjini hapa huku akibainisha kuwa, misimamo ya aina hiyo itasababisha wananchi ambao wanakipenda chama hicho miaka mingi kujenga chuki.

“Sisi kupitia Halmashauri Kuu Iringa Mjini na chama kwa ujumla hatukumtuma Diwani Mheshimiwa Edward, kwenda kuhamasisha wananchi kuchapwa viboko, tulimtuma kwenda kuwaunganisha wananchi na kuisimamia Serikali ili kupeleka maendeleo kwa kasi katika Kata ya Mwangata.

“Sasa kauli za namna hii zinapotolewa na kiongozi ambaye anaheshimika zinatafsriwa kwa namna tofauti, atambue kuwa suala la kushiriki msiba ni hiyari ya mtu,na wala si lazima na Chama Cha Mapinduzi kinaheshimu wananchi wote bila kujali kabla, dini au itikadi zao,ndiyo maana tumejikita sana katika suala la utu, utii na heshima kwa wote, hivyo kauli tata namna hii zinapotolewa wakati mwingine zinaweza kusababisha maumivu,hivyo ni busara afute kauili hiyo ya wasioudhuria misiba wachapwa viboko,”amesema Mgongolwa.

kwa kina zaidi soma gazeti la majira leo juni 8, popote ulipo tanzania